BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UMISSETA UNAVYOIBUA VIPAJI VYA MICHEZO MBALIMBALI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO.


Mshambuliaji wa kanda ya Kihonda B, Emelina Aman kulia akiwania mpira dhidi ya beki wa kanda ya Sua, Emelina Aman wakati wa mchezo wa soka kwa wasichana katika mashindano ya kusaka wachezaji wakuunda vikosi vya umoja wa michezo shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 yanayoendelea katika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

 Moja wa wasichana wakichuana katika mbio za mita 400 kwenye uwanja huo wa Jamhuri.
 Wanafunzi wa kanda ya Mjini Kati wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya umoja wa shule za sekondari Tanzania ambapo wanafunzi zaidi ya 750 wanashiriki mashindano hayo kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Wanafunzi wa kanda ya SUA
Wanafunzi wa kanda ya Tungi

 Wanafunzi wa kanda ya Kihonda B

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo amewataka wakufunzi na walimu wa michezo mbalimbali katika mashindano ya umoja wa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) kuwa makini wakati wa kuchagua wachezaji wa wilaya ya Morogoro ili kusaidia kupata wachezaji wazuri wataowakilisha vema mashindano ngazi ya mkoa huo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ngazi ya halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika uwanja wa jamhuri mjini hapa, Nondo alisema kuwa ili kupata wachezaji wazuri wa kuwakisha michezo ya Umisseta ngazi ya mkoa ipo haja kwa wakufunzi na makocha kuwa makini wakati wa kuangalia wachezaji ambao wataunda vikosi vya michezo mbalimbali katika mashindano hayo.

Nondo alisema kuwa mashindano hayo ni mazuri sana na lengo la kuanzishwa kwake ni kuibua vipaji vilivyojificha na kuviendeleza hivyo wakufunzi hapo wanahitajika kuwa makini katika kuangalia vijana hao kwa kila mchezo ili timu zitakazoundwa za wilaya ya Morogoro ziwe imara na kutwaa ushinda na hiyo itasaidia sana wachezaji wengi wenye vipaji kupata nafasi ya kuendeleza kwenye hatua zinazoendelea.

“mashindano haya ya Umisseta ni mazuri sana kwani yamekuwa yakiibu wachezaji wenye vipaji vingi vya kila aina ya mchezo hivyo umakini wa wakufunzi na makocha wa kuchagua wacvhezaji unahitajika sana ili Manispaa tupate timu imara” alisema Nondo.

Aliongeza kuwa ukiwa na wachezaji wazuri lazima utakuwa na timu imara lakini itakuwa faida kubwa  kwa wachezaji hao kupata nafasi mzuri ya kuendelea kuonyesha vipaji vyao.

Naye Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro, Asteria Mwang’ombe alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha jumla ya kanda sita ambazo katika kanda zao tayari zilifanya michezo na kupata wachezaji ambao wameunda vikosi vya timu mbalimbali.

Mwang’ombe alitaja michezo ambayo inashindaniwa ni pamoja na soka, netiboli, baskeboli, bao, mpira wa wavu, meza, riadha, na taaluma ambazo washiriki wanatoka katika kanda sita za shule za sekondari za Mjini kati, Bigwa, Kihonda A, Sua, Kihonda B, na Tungi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: