BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NYUMBA YA MKUU WA POLISI WILAYA YA RUFIJI (OCD) YAVUNJWA BAADA YA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI.

HALI bado siyo shwari Ikwiriri wilayani Rufiji, baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), kuivunja na kuharibu mali huku wengine wakichoma moto magari na nyumba wananchi.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa, vurugu hizo ziliibuka usiku wa kuamkia jana kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji eneo hilo.

Wakati hayo yakiendelea, watu 49 kutoka jamii ya wafugaji wamehamia na kuishi na familia zao Kituo cha Polisi Ikwiriri, kuepuka vurugu zinazoendelea mitaani ambazo juzi ziliripotiwa kupoteza maisha ya mkulima mmoja.

Ingawa polisi wanasema hali ni shwari, taarifa zilizothibitishwa na watendaji wa chini zinaeleza siyo shwari na wakati wowote vurugu zinaweza kurudi tena.

Katika eneo la Ikwiriri inakopita barabara kuu ya Dar es Salaam- Mtwara, jana biashara ya maziwa iliyokuwa ikifanywa na wake wa wafugaji haikuwapo, inadaiwa wamehofia usalama wao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema hadi saa 4:00 asubuhi jana hali ilikuwa shwari na kwamba, wanaendelea kufanya doria za ili kujiridhisha.

Pia, Mangu alisema lengo la doria hizo pia ni kuhakikisha kinachosemwa na baadhi ya watu kuwa, kuna dalili za kurejea vurugu iwapo ni kweli au la.

Mangu alisema hadi jana asubuhi walikuwa wanashikilia watu 50 kwa tuhuma za kufanya vurugu, ikiwamo kufunga barabara na kuharibu mali kadhaa.

Alisema wanaoshikiliwa siyo wafugaji wala wakulima, hivyo kama kuna taarifa za kuwapo ulipizaji kisasi siyo sahihi kwani kati ya makundi hayo hakuna kundi lililochukuliwa zaidi ya vijana wa mjini waliokuwa wakifanya vurugu.

“Sisi hatujawakamata wafugaji au wakulima, katika operesheni ilikuwa ya kukamata watu waliokuwa wakifanya vurugu ndiyo tunaowashikilia, sasa ukisema kuna madai ya wafugaji kutaka kulipiza kisasi hapo nashangaa kwa maana mbili, kwanza siku ya fujo hakuna hata mfugaji mmoja aliyelipiza kisasi kwa mkulima,” alisema Mangu na kuongeza:

“Kweli wafugaji walionyesha kutii walau sheria kwa sababu, licha ya baadhi ya watu kudai wakulima wanawashambulia, wao walikuwa hawajajibu mashambulizi ndiyo maana vurugu hizi tumeweza kufanikiwa kuzizima mapema, lakini kama wafugaji nao wangeenda kuwapiga wakulima hapo sasa kazi ingekuwa ngumu.”

Kuhusu madai ya ofisa mmoja wa jeshi hilo kuhamishwa kituo cha kazi siku hiyo ya tukio, Mangu alisema hana taarifa hizo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: