BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKACHERO WA JESHI LA POLISI WALIVYOMNASA MWIZI WA VYOMBO VYA NDANI MANISPAA YA MOROGORO

ASKARI kanzu wa kikosi cha upelelzi katika jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wakiwa na mtuhuwa wa wizi mali mbalimbali Joseph Chewe (mwenye sharti nyekundu) zilizopo chini mara baada ya kukamatwa katika nyumba anayoishi eneo la Kiwanja wa Ndege-Ujenzi kwa tuhuma za kumuibia mwanafunzi wa chuo cha Ujenzi Morogoro vyomba mbalimbali muda mfupi kabla ya kumpeleka kituo kikuu cha polisi mtaa wa Kitope mkoani hapa.
 Mmoja wa makachero wa kitengo cha upelelezi akivunja mlango ili kuweza kuingia ndani kutoa mali za wizi zinazodaiwa kuibwa na kijana Joseph Chewe wa kwanza kulia anayeshuhudia tukio hilo.
 Sakari hao wakiorodhesha vifaa mbalimbali vikiwemo vya muziki na begi la nguo baada ya kuvunja mlango na kuingia ndani na kufanikiwa kukuta baadhi ya mali hizo huku mtuhumiwa anayedaiwa kutenda uharifu Joseph Chewe wa pili kutoka kulia akiangalia zoezi hilo linavoendeshwa.
 Hapa Joseph Chewe akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu Nicolaus Kabipe mwenye fulana la pundamilia na vijana wengine walioamua kusaidia kubeba mali zilizokamatwa na askari hao wakati wa zoezi hilo lilidumu kwa zaidia ya saa moja.
 Hapa Joseph Chewe akitia saini mali anazodaiwa kuiba katika kitabu ambacho kimeorodheshwa mali hizo chini ya askari kanzu Nicolaus Kabipe kushoto muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea kituo kikuu cha polisi mkoani hapa.
 Askari wa kikosi cha pikipiki  katika Manispaa ya Morogoro chini ya afande Mwajabu Juma kulia wakisimamamia zoezi la ulinzi kwa mtuhumiwa Joseph Chewe kabla ya kupelekwa kituo cha polisi.
Mtuhumiwa wa tukio hilo, Joseph Chewe akielekea kupanda gari (halipo pichani) ili kwenda kituo cha polisi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: