Morogoro Secondary teacher salvages some bags from a burning girls' dormitory. The fire incident, which happened early yesterday, destroyed the dormitory and most of the students' belongings, The cause of the fire was not immediately established. Polisi are investigating the incident.
Baadhi ya wanafunzi wakipekua masalia katika mabegi ya chuma baada ya kutokea ajali ya moto katika bweni la wasichana la Morogoro Sekondari.
Bweni la wasichana linavyoonekana kwa ndani baada ya tukio hilo kwa moto kuteketeza vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na wasichana hao.
Wanafunzi wakiwa katika hospitali ya rufaa ya Morogoro muda mfupi baada ya kufikishwa kutokana na baadhi yao kuzimia na kukimbizwa ili kuweza kupatiwa huduma ya kwanza wakati wakiwa ndani ya Bweni hilo.
Mmoja wa wazazi akimpatia soda msichana katika hospitali ya rufaa kufuatia baadhi ya wanafunzi kuzimia kutokana na moshi wakati bweni lao likitekete kwa moto huku wakisubiri huduma ya kwanza.
Askari wa kikosi cha zimamoto wakimalizia kazi ya kuzima moto huo.
Jengo la Bweni la wasichana shule ya sekondari ya Morogoro ambalo lilikuwa linakaliwa na wasichana zaidi ya 30 kwa ajili ya malazi linavyoonekana baada ya kutokea kwa tukio hilo julai 16 usiku majira ya saa 1:45 mwaka huu.








0 comments:
Post a Comment