RIPOTI ya Shirika la Umoja wa Mataifa imesema Eritrea imepunguza
msaada wake kwa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab nchini Somalia
kutokana na shinikizo la kimataifa, lakini bado inakiuka maazimio ya
Baraza la Usalam.
Kundi la Uangalizi la Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia na Eritrea,
ambalo linachunguza ukiukaji wa vikwazo vya silaha dhidi ya nchi hizo
mbili, limesema katika ripoti yake lililowasilisha kwa Baraza la Usalama
kuwa halikupata ushahidi wa msaada wa moja kwa moja wa Eritrea kwa
al-Shabaab katika kipindi cha mwaka uliopita.
Mji wa Mogadishu umeshuhudia mashambulizi mengi ya wanamgambo wa kujitoa mhanga.
Ripoti hiyo inasema ijapokuwa inawezekana kuwa maafisa wa Eritrea
wanaendelea kutoa usaidizi wa kifedha na mbinu nyingine za msaada kwa
makundi ya upinzani nchini Somalia, bila shughuli zao kugundulika, kundi
la Uangalizi linatathmini kuwa usaidizi wa aina yoyote kama huo ni
mdogo.
Badala yake jopo hilo liliwasilisha ushahidi kuwa Eritrea iliwatuma
waasi wa Ethiopia kupitia Somalia, ikayauzia makundi haramu silaha
nchini Sudan ambayo hufanya biashara na wafanyabiashara wa silaha wa
Palestina na ikaagiza kutoka ng'ambo vipuri vya jeshi lake la angani.
Aidha ripoti hiyo ilidai kuwa waasi wa kabila la Afar waliohusika na
mauaji ya watalii watano wa Ulaya Kaskazini mwa Ethiopia mwezi wa
Januari mwaka huu walipewa hifadhi na mafunzo nchini Eritrea, ijapokuwa
hakukuwa na ushahidi kuwa nchi hiyo ya bahari ya shamu ilikuwa na jukumu
la moja kwa moja katika mauaji hayo.
Iliishutumu Eritrea kwa kukataa kukubaliana na maazimio ya Baraza la
Usalama na inaendelea kuwa na ushawishi mbaya na kufanya uharibifu
katika kanda hiyo.
Kanisa la African Inland lililoshambuliwa kwa gurunedi mjini Gariss.
Nchi hiyo awali imekanusha madai hayo na ikatoa wito wa kubadilishwa
wanachama wa jopo hilo kuhusu kile inakiita kuwa ni wanaipendelea
Ethiopia ambayo ni hasimu wake mkuu.
Wajumbe wa Eritrea katika Umoja wa
Afrika walikataa kuzungumzia ripoti hii ya Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo Umoja wa Afrika –AU umelitaja shambulizi la bomu nchini
Somalia ambalo lilisababisha kifo cha mbunge mmoja na kuwajeruhi watu
watano kuwa ni kitendo cha “uwoga” kilicholenga kuhujumu mchakato wa
amani katika nchi hiyo inayokumbwa na vita.
Mohamed Abdinur Garweyne aliuawa katika mripuko huo uliotokea mjini Mogadishu, ambao kundi la al-Shabaab lilikiri kuhusika.
Kwingineko polisi watatu wa Kenya wameuawa katika shambulizi
lililofanywa Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Somalia jana
Jumatatu.
Kenya imekumbwa na msururu wa mashambulizi ya gurunedi na mabomu tangu
vikosi vyake vilipovuka mpaka na kuingia nchini Somalia mwezi Oktoba
mwaka jana na imelilaumu kundi la al-Shabaab, na wale wanaoliunga mkono
kundi hilo ndani ya Somalia.
Mkuu wa polisi wa jimbo la Garissa George
Kingi alisema Polisi hao watatu waliuawa wakiwa safarini kuelekea eneo
la Liboi.
KWA MSAADA WA SHIRIKA LA DW.


0 comments:
Post a Comment