BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA ITACHUKUA HATUA DHIDI YA SERIKALI ENDAPO ITAENDELEA KUKINYANYASA CHAMA HICHO.

 Katibu mkuu wa chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Willbrord Slaa akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya kuhaghailisha mkutano wa hadhala wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) katika mkoa wa Iringa ambao ulitarajiwa kufanyika leo ambapo mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika hoteli ya Mount Uluguru mkoani Morogoro. kulia ni Kaimu Katibu mkuu Chadema Zanzibar, na kushoto ni Mkuu wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) Benson Kigaiya.
 Mkuu wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) Benson Kigaiya akifafanua jambo katika kutano huo kuliqa ni
 Katibu mkuu  (CHADEMA) Dkt Willbrord Slaa na kushoto ni Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu.


 NCHI ya Tanzania siku moja baada ya polisi kuzuia maandamnao ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chedema mjini Morogoro na Iringa ikiwemo kushutumiwa kwa kuua mtu mmoja kwa kumfyatulia risasi, serikali imesema kuwa inachunguza tuhuma dhidi ya Jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mtu huyo.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi alieleza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jumanne kwamba kuna utata wa  namna kifo hicho cha mtu huyo anayesadikiwa kupigwa risasi na polisi kwa kuwa polisi mkoani Morogoro inasema ilipata taarifa za kuwepo mtu mmoja aliyejeruhiwa kichwani mita 300 kutoka eneo la tukio.


Waziri Nchimbi ametoa sababu ya polisi kuzuia maandamano hayo ya Chadema na kusababisha kupambana na wafuasi waliolazimisha kuandamana kabla ya kufanyika mkutano wa hadhara wa chama hicho mjini Morogoro.


Waziri huyo alitoa wito kwa vyama vya siasa nchini kufuata sheria na taratibu za nchi wakati wa kufanya shughuli zao za kisiasa.


Wakati huo huo katibu mkuu wa Chadema Dk. Willbroad Slaa katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Morogoro jana alilishutumu jeshi la polisi kuwa linahusika katika mauaji ya kijana aliyekufa wakati wa maandamano ya chama hicho aitwae Ally Zona kwa kuwa lilitumia hatua zisizofaa za kulazimisha kuzuia maandamano hayo ya amani kinyume cha sheria na taratibu za nchi.


Dk. Slaa amesema Chadema inasubiri taarifa ya  daktari anayefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu ili kuweza kuchukua hatua za kisheria.


Alipotakiwa kuzungumzia suala la kuhusika au kutohusika kwa jeshi la polisi katika mauaji ya kijana huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile amesema jeshi lake litatoa tamko rasmi jumatano hii.


kutokana na kuchelewa kukamilika kwa uchunguzi wa kitaalamu wa madakatari kuhusiana na kifo hicho.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: