Christof Heyns.
MWAKILISHI maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yaliyo ya
halali au kunyonga kiholela, Christof Heyns ameitaka serikali ya Gambia
kujizuia na kutotekeleza mauaji ya watu 39 ambao wako kwenye orodha ya
waliohukumiwa kifo, kufuatia kunyongwa kwa watu tisa Agosti 26 mwaka
huu.
Kabla ya mauaji haya utekelezaji wa hukumu ya kifo ya mwisho rasmi
katika nchi hiyo ulifanyika mwaka 1985.
Mwakilishi huyo amesema analaani vikali unyongaji huo ulitekelezwa
wiki iliyopita nchini Gambia na kuitaka serikali isitekeleze mauaji
zaidi.
Amesema mauaji hayo ni hatua ya kurudi nyuma katika suala la
kulinda haki ya kuishi duniani.
Ameongeza kusema utekelezaji wa hukumu
ya kifo ni ukandamizaji wa hatua nzuri zilizokuwa zimepigwa katika
kuelekea kukomesha hukumu ya kifo Gambia.
Hata hiyo Rais Yahya Jammeh wa
nchi hiyo amepanga kuhakikisha kwamba hukumu hiyo ya kifo inatekelezwa katika wiki chache zijazo.
0 comments:
Post a Comment