Wachimba migodi wa Marikana waliokamatwa.
WENDESHA mashtaka wa serikali nchini Afrika Kusini
wanasema kuwa wanajianda kuwafungulia mashtaka ya mauaji wachimba migodi
wa mgodi wa Marikana.
Ripoti zinasema pia, wachimba migodi hao,
wanakabiliwa na mashtaka mengine ikiwemo jaribio la mauaji ya wachimba
migodi thelathini na wanne ambao waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Msemaji wa ofisi ya kiongozi wa mashtaka nchini
humo, amesema ikiwa watu, ambao baadhi yao wamejihami wakiwakabili
polisi na kutokee mauaji, wale watakaoshikwa na polisi watafunguliwa
mashtaka ya mauaji, bila kujali wale waliofyatua risasi.
Polisi waliwapiga risasi wachimba migodi hao kufuatia ghasia na maandamano kuhusu mishahara.
Maafisa wawili wa polisi waliuawa kwenye machafuko hayo.
0 comments:
Post a Comment