ANGELA MERKEL KUSHOTO NA FRANCOIS HOLLANDE KULIA.
Msemaji wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa
mkutano huo utakaofanyika katika mji wa Ludwigsburg kusini
magharibi mwa Ujerumani , ambako De Gaulle alitoa hotuba hiyo kwa
vijana wa Ujerumani katika hatua muhimu ya maridhiano baada ya
vita vikuu vya pili vya dunia, utakuwa tu kwa kiasi kikubwa
kwa ajili tu ya heshima za sherehe za maadhimisho.
Lakini mada chache muhimu hata hivyo zitakuwa katika agenda ya majadiliano.
Suala la kampuni la kuunda vyombo vya usafiri wa anga la
EADS na lile la Uingereza la BAE bila shaka litazungumzwa katika
chakula cha mchana kitakachotumiwa kufanya majadiliano hayo
pamoja na rais Francois Hollande, msemaji huyo , Steffen Seibert,
amewaambia waandishi habari Ijumaa, (21.09.2012), akilenga kuhusu
mkutano huo ambao haukutangazwa sana.
Kampuni ya Uingereza ya BAE inazungumza na EADS kutana kuungana.
"Bila shaka hakutakuwa na maamuzi Jumamosi hii na msiende
katika mkutano huo wa waandishi habari mkitarajia kutakuwa na
jambo lolote la maamuzi," alisema Seibert.
Hii pia itakuwa pamoja
na suala la udhibiti mkali wa sekta ya benki katika bara la
Ulaya , mtazamo wa mapambano dhidi ya mzozo wa madeni katika
eneo la euro kwa wakati huu, Seibert amesema.
Serikali zimekuwa zikichukua tahadhari tangu kutangazwa wiki
iliyopita kuwa kampuni ya vifaa vya ulinzi nchini Uingereza BAE
na kampuni linayotengeneza ndege katika bara la Ulaya EADS
yanafanya majadiliano ya kuungana.
Rais wa Ufaransa amesema kuwa Paris na Berlin zinasubiri mradi
huo wa kuungana kufafanuliwa kabla ya kupitisha maamuzi na
kuchukua uamuzi.
Ujerumani pia imechukua msimamo wa kusubiri na kuona, huku
baadhi ya maafisa wakitia shaka kuwa muungano huo unaweza
kusababisha ukosefu wa ajira.
Kampuni inayounganisha ndege za Airbus EADS A320
Makampuni hayo mawili yamepewa hadi Oktoba 10 kukamilisha mradi
wao ama waachane nao.
Ujerumani na Ufaransa zina hisa nyingi
katika kampuni la EADS, wakati serikali ya Uingereza ina hisa
kubwa katika kampuni la BAE ambazo zinairuhusu kutumia kura ya
turufu kuzuwia maamuzi ambayo inayaona kuwa hayaendani na maslahi
ya umma.
Wakati Ufaransa inapendelea kutoa madaraka kwa benki kuu ya
Ulaya kuangalia benki zote 6,000 za eneo la mataifa ya euro
kuanzia mwezi Januari, Ujerumani inataka kuziangalia benki kubwa
tu na haiko katika hali ya kuharakisha, ikipendelea udhibiti wa
kina kwanza badala ya haraka.
Sherehe za Jumamosi ni za hivi karibuni kabisa katika wimbi la
matukio ya maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya
mahasimu hao wa wakati wa vita.
Merkel na Hollande watakutana katika kasri la Baroque mjini
Ludwigsburg, watatoa maelezo kidogo na kisha watarejea katika
shughuli za majadiliano pamoja na kupata chakula cha mchana.
Viongozi hao , ambao wanajaribu kuweka msuguano wao katika
kiwango cha chini tangu rais Hollande kuingia madarakani mwezi
Mei, wanatarajia kuwa na mkutano wa pamoja na waandishi habari
mchana.

0 comments:
Post a Comment