WAPIGANAJI waliojihami kwa Bunduki walivamia Gereza moja katika mji wa Tikrit nchini Iraq na kuwauwa askari jela kumi na wawili kabla ya kutorosha idadi isiyojulikana ya wafungwa.
Afisa mmoja alithibitisha kuwa Maafisa hao wa
Polisi waliuawa katika gereza la Tasfirat lililovamiwa na wapiganaji hao
na kusema hali imedhibitiwa kwa hivi sasa na maafisa wa usalama.
Shambulizi hilo lililoanza kwa mlipuko wa bomu
lilotegwa kwenye gari nje ya lango kuu, lilitekelezwa usiku kucha hadi
alfajiri ya ijumaa.
Gereza hilo linawahifadhi mamia ya wafungwa wakiwemo wale wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Al-Qaeda.
Sheria ya kutotoka nje imetangazwa katika mji wa Tikrit kufuatia uvamizi huo.
0 comments:
Post a Comment