MWANAFUNZI mmoja wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Msiliembe mkoani Tabora amekufa hapo hapo na wengine 23 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi.
Majeruhi watano miongoni mwa hao, wamelezwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora ya Kitete, kwa matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Edward Bukombe, alisema tukio hilo Septemba 25 mwaka huu ,katika Kijiji cha Msiliembe, wilayani Uyui.
Kaimu kamanda huyo alimtaja aliyekufa kuwa ni, Husna Ramadhani (10) na kwamba radi hiyo ilipiga wakati watoto hao wakiwa darasani.
Bukombe alisema katika siku hiyo kulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na radi.
Alisema katika tukio hilo, watoto wengine 23 walipata madhara, lakini watano walijeruhiwa vibaya na kukimwizwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Aliwataja waliolazwa kuwa ni Bundala Juma (10) ,Hamisi Mashaka (10), Cresesia Simon (12) Kwangu Luone (12) na Zaituni Ally (10).
Alisema hata hivyo hali za wanafunzi zinaendelea vizuri kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa daktari wa mkoa .
0 comments:
Post a Comment