BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA CHAMTAKA IGP KUUNDA TUME HURU KUCHUNGUZA VIFO VINAVYOTOKEA KATIKA MAZINGIRA YA UTATA NDANI YA JESHI LA POLISI.



KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, kuunda tume huru ya kushughulikia vifo vinavyotokea katika hali za utata, hasa vinavyohusisha jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kumaliza kikao chake na IGP Mwema, Dk. Slaa alisema wamemwambia ikiwa Jeshi la Polisi litaendelea kung’ang’ania kujichunguza katika matukio ya kihalifu huku wakiwa ndio watuhumiwa, CHADEMA hakitakuwa tayari kutoa ushirikiano.

“Tulimwambia ni lazima sheria zifuatwe na haziwezi kufuatwa kama polisi watajichunguza wenyewe kwa maana katika hatua hii ya awali tayari wamekwisha kuonesha hali ya kutoaminika kwa kusema milipuko ile ilibebwa na waandishi wa habari,” alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa katika hatua hiyo ya awali walikubaliana na IGP Mwema kuunda kamati ya kufuatilia na kupokea malalamiko.

Kwa upande wa CHADEMA ameteuliwa, Tumaini Makene huku kwa upande wa Polisi atakuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba na kamati hiyo imeanza kazi jana.

Alisema kuwa makubaliano mengine ni IGP kuruhusu mikutano ya ndani ya CHADEMA kuendelea na kutoa amri kwa askari wa mkoa wa Iringa kuruhusu watuhumiwa waliokamatwa katika tukio hilo kupelekewa chakula.

Aliongeza kuwa katika makubaliano hayo walimueleza IGP kuhakikisha kila maelezo yake yanayofanyika kati yao na CHADEMA yanakuwa katika maandishi kwa kile alichoeleza kuwa mara nyingi walipokubaliana na polisi wamekuwa wanageuka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: