BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHINA YAZINDUA MONAWARI YA KWANZA INAYOBEBA NDEGE ZA KIVITA.

MANOWARI ya kwanza ya China inayobeba ndege za kivita, imekabidhiwa kwa Jeshi la Majini la Umma la China hii leo baada ya kufanyiwa marekebisho na majaribio kwa muda mrefu.

Mbele ya rais Hu Jintao wa China na Waziri mkuu Wen Jiabao, mkandarasi mkuu alikabidhi rasmi manowari hiyo kwa jeshi la wanamaji kwenye hafla iliyofanyika katika kambi ya jeshi la umma iliyoko mjini Dalian, kaskazini mashariki mwa China.

Rais Hu Jintao, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi nchini China, aliweka bendera ya Jeshi la ukombozi wa umma la China, na kutoa hati kwa kikosi cha jeshi la majini kilichopokea manowari hiyo.

Rais Hu alipata fursa ya kutembelea meli hiyo na kukagua gwaride la heshima la kikosi cha jeshi la majini la China.

Rais Hu amepongeza ujenzi wa manowari ya Liaoning, ambayo awali iliitwa Soviet Varyag, na kuliamuru jeshi la majini na vyuo husika vya utafiti kuendelea na kazi nzuri wanazofanya.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Wen Jiabao amesema utengenezaji wa manowari hiyo ni uamuzi muhimu uliofikiwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China, Baraza la serikali la China na Kamati Kuu ya kijeshi.
 
Ameongeza kuwa manowari hiyo inaongeza nguvu ya ulinzi wa taifa na kuonyesha nguvu ya jumla ya nchi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: