Mamia ya maduka yameungua moto katika soko la kale mjini Aleppo
Jumamosi mwaka huu wakati mapigano baina ya waasi na majeshi ya
serikali, yanatishia kuharibu eneo hilo lililotengwa na UNESCO kuwa
turathi ya dunia.
Vuguvugu la mageuzi lililogeuka kuwa vita vya wenyewe kwa
wenyewe ambavyo vinaendelea hivi sasa nchini Syria vimesababisha
watu 30,000 kupoteza maisha yao, kwa mujibu wa makundi ya
wanaharakati nchini Syria kama kundi linaloangalia haki za
binadamu nchini humo lenye makao yake makuu mjini London.
Lakini mbali na gharama ya upotevu wa maisha ya watu , lakini
nyingi ya hazina za kihistoria pia zimeharibiwa katika mzozo huo
uliodumu sasa miezi 18, ambao umeyaacha baadhi ya maeneo ya
miji kuwa magofu.
Soko ambalo ni turathi za dunia mjini Aleppo likiungua moto.
MASHAMBULIZI MAPYA MJINI ALEPPO.
Wapiganaji wanaopigana kumwondoa madarakani rais Bashar al-Assad
wametangaza kuwa wamefanya shambulio jipya dhidi ya mji wa
Aleppo, mji wa kibiashara wa Syria wenye wakaazi wapatao milioni
2.5, siku ya Alhamis, lakini hakuna upande unaoonekana kupata
ushindi.
Mjini Aleppo , wanaharakati wakizungumza kupitia mtandao wa Skype
wamesema wanajeshi wa serikali waliokaa katika maeneo maalum
wakiwalenga watu shabaha, wanafanya hali kuwa ngumu kwa wao
kukaribia eneo la Souk al-Madina, soko la kale lenye njia
nyembamba lililoko katika mji mkongwe, ikiwa ni moja kati ya
vivutio vikubwa vya utalii.
MAPIGANO YAMEACHA BAADHI YA MAENEO KUWA MAGOFU MJINI ALEPPO.
SOKO LAUNGUA.
Video vizilizowekwa katika tovuti ya You Tube katika mtandao wa
internet , zinaonesha wingu kubwa jeusi likitanda katika anga la
mji huo.
Wanaharakati wamesema kuwa moto umezuka kutokana na mashambulio
ya makombora na risasi siku ya Ijumaa na wanakadiria kuwa kati
ya maduka 700 hadi 1,000 yameharibiwa hadi sasa. Maelezo hayo
ni vigumu hata hivyo kuweza kuthibitishwa, kwasababu serikali
inazuwia vyombo vya habari vya kimataifa.
WAPIGANAJI WA JESHI LA WAASI MJINI ALEPPO.
Mji mkongwe uliopo mjini Aleppo ni moja kati ya maeneo
yaliyotengwa na shirika la umoja wa mataifa ya sayansi na
utamaduni UNESCO, kuwa turathi ya dunia, ambapo hivi sasa umo
katika hatari kutokana na mapigano hayo.
MAENEO MENGINE HATARINI.
UNESCO inaamini kuwa maeneo matano kati ya sita ya turathi
nchini Syria , ambayo pia ni pamoja na mji wa kale uliopo
jangwani wa Palmyra na sehemu za mji mkongwe mjini Damascus
yameathirika.
MAPIGANO YAENDELEA NCHINI SYRIA.
Shirika la kuangalia haki za binadamu nchini Syria lenye makao
yake makuu mjini London , ambalo linamtandao wake wa wanaharakati
nchini Syria , limesema kuwa majeshi ya Assad na waasi
wanalaumiana kila mmoja kwa kuzusha moto huo.
0 comments:
Post a Comment