BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAKALA LA FILAMU YA KIMAREKANI NA VIJIKATUNI VYA UFARANSA VYAIKASIRISHA WAISLAM DUNIANI, WAANDAMANA KILA KONA YA DUNIA KUZILAANI NCHINI HIZO.

 MAANDAMANO ya kupinga filamu ya Kimarekani na vijikatuni vya Kifaransa vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) yameendelea kufanyika katika nchi mbalimbali duniani.

Yalifanyika baada ya sala za Ijumaa  yameshuhudiwa nje ya balozi za Ufaransa na Marekani katika miji mbali mbali ya  Misri, Lebanon, Pakistan, Yemen, Libya, Tunisia, Indonesia, Bangladesh, Saudi Arabia  ikiwemo na Tanzania

Miji ya Iran pia imeshuhudia maandamano makubwa ya kulaani vitendo vya kumvujia heshima Mtume SAW. 

Waandamanaji walipiga nara za "mauti kwa Marekani", "mauti kwa Israel"  "mauti kwa Ufaransa" na "mauati kwa Uingereza".

Aidha katika maandamano hayo kote duniani, Waislamu wametangaza mahaba yao kwa Mtume wa rehma Mohammad SAW na kusema wako tayari kujitolea mhanga kwa ajili ya kumtetea
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: