POLISI wa Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa
mwanasiasa wa hiyo anayeleta utatanishi, Julius Malema ambaye
alifukuzwa kutoka chama tawala cha ANC.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo kuhusu mashtaka ya ku-ghu-shi fedha, rushwa, na wizi kwa njia za udanganyifu.
Kamati maalumu ya uchunguzi, iitwayo "the Hawks", imekuwa ikichunguza shughuli za kibiashara za Malema.
Malema, ambaye aliwahi kuwa mfuasi mkubwa
wa Rais Jacob Zuma, amegombana na washirika wake wa zamani, na
akafukuzwa chamani, kwa kutoa wito kuwa serikali ya Botswana inafaa
kupinduliwa.

0 comments:
Post a Comment