RAIS Barack Obama wa Marekani amedai kwamba baada ya kupitisha
muongo mzima wa kupigana vita, Marekani hivi sasa ina nguvu zaidi na
inaheshimiwa duniani kote.
Akitoa hotuba kwa mnasaba wa kutimia
mwaka wa pili tangu kumalizika operesheni za kijeshi za Marekani nchini
Iraq, Obama amedai, wanamaliza muongo mmoja wa vita huku wakiwa
wamesambaratisha mitandao ya kigaidi iliyowashambulia hatua ambayo
amedai imezidi kuutia nguvu uongozi wa Marekani.
Obama amesema hivi sasa
kila Mmarekani anaona fakhari kwamba nchini humo kuna usalama na kwamba
eti Marekani ina nguvu na inaheshimiwa zaidi duniani.
Aidha Obama ametoa
matamshi hayo hali ya kuwa, kuongezeka idadi ya askari wa Marekani
wanaouawa na kujeruhiwa Afghanistan kunazidisha hasira za wananchi wa
Marekani na wa nchi wanachama wa NATO, na hivyo kuongeza hisia za
kupinga siasa za kupenda vita za watawala wa Marekani.
0 comments:
Post a Comment