
VITA nchini Syria ,hali ya wasi wasi inayoongezeka kuhusiana na
mpango wa Iran wa kinuklia na maandamano ya Waislamu dhidi ya mataifa
ya magharibi, vitaweka kiwingu katika mkutano wa umoja wa mataifa.
Maneno ya tahadhari pamoja na ukaidi yanatarajiwa wakati rais
wa Marekani Barack Obama , kiongozi wa Iran Mahmoud Ahmedinejad na
waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu watakapojiunga na zaidi
ya viongozi 120 wa mataifa na serikali katika baraza kuu la
umoja wa mataifa.
Kwa sababu ya mgawanyiko mkubwa wa kimataifa kuhusiana na mzozo
uliodumu sasa miezi 18 nchini Syria , umoja wa mataifa hautakuwa
na mkutano rasmi kuhusiana na vita hivyo vya wenyewe kwa
wenyewe.
OBAMA KUHUTUBIA KWANZA.
Lakini rais Obama na viongozi wa mataifa ya magharibi
wanatarajiwa kutoa wito wa kuchukuliwa hatua katika hotuba zao.
Rais wa Marekani ni mmoja kati ya wazungumzaji wa mwanzo siku
ya Jumanne asubuhi baada ya tukio hilo kufunguliwa na katibu
mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Na kampeni dhidi ya Syria itaendelezwa nje ya baraza kuu la
umoja wa mataifa.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na mataifa ya
Kiarabu, Arab League Lakhdar Brahimi atatoa maelezo katika baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa kesho Jumatatu kuhusiana na
mazungumzo yake na rais Bashar al-Assad.
Syria pia inakuwa mada kuu katika baraza la usalama wakati wa
mjadala wa mawaziri kuhusiana na Arab League siku ya Jumatano,
umoja wa ulaya unatarajiwa kuanzisha wito mpya kwa ajili ya
mfuko wa fedha za huduma ya kiutu na mkutano wa mawaziri wa
marafiki wa Syria unapangwa kufanyika siku ya Ijumaa.
MAJERAHA YA KIDIPLOMASI.
Majeraha ya kidiplomasia kuhusu Syria hayako karibu na kupata
nafuu. Si Urusi ama China , nchi ambazo zimetumia kura zao za
turufu mara tatu kuzuwia maazimio ya baraza la usalama kuhusu
Syria , zitawakilishwa na viongozi wa ngazi ya juu mjini New
York.
RAIS OBAMA.
ASSAD anatarajiwa kumtuma waziri wake wa mambo ya kigeni.
"Kila mmoja atakuwa anafikiri kuhusu Syria, atazungumza kuhusu
Syria , lakini hakutakuwa na uamuzi na hakuna hatua kubwa
itakayopigwa," amesema mwanadiplomasia mmoja mwandamizi wa umoja
wa mataifa, akizungumza kwa mashariti ya kutotajwa jina.
Stewart Patrick , mtaalamu wa taasisi ya kimataifa inayokusanya
mawazo kuhusu utawala wa dunia kwa ajili ya baraza la uhusiano
wa kimataifa , amesema hata hivyo kuwa Syria itakuwa moja ya
masuala yanayopewa umbele katika baraza kuu la umoja wa mataifa
pamoja na mvutano kuhusu Iran.
Ahmedinejad yuko mjini New York
huenda kwa mara yake ya mwisho kuonekana katika baraza kuu.
WASI WASI WAZIDI.
HALI ya wasi wasi wa usalama pamoja na diplomasia zaidi
vinatarajiwa huku kukiwa na uvumi mkubwa kuwa Israel inapanga
kuishambulia kijeshi Iran katika maeneo yake ya kinuklia ambapo
Iran inasisitiza kuwa ni kwa ajili ya matumizi ya amani, lakini
mataifa ya magharibi yanasema nchi hiyo inaficha majaribio ya
kutengeneza bomu la nuklia.
Ahmedinejad atazungumza katika baraza kuu siku ya Jumatano,
wakati hatua mpya ya mataifa kadha kutoka katika ukumbi huo
ikitarajiwa iwapo kiongozi huyo wa Iran atarejea matamshi yake ya
kuishambulia Israel.
Rais wa Iran Mahmud Ahmadinejad.
MAAFISA wa ngazi ya juu kutoka Uingereza, China, Ufaransa,
Ujerumani, Urusi na Marekani , ambao wanajaribu kujadiliana na
Iran, wanatarajiwa kukutana siku ya Alhamis mara tu baada ya
waziri mkuu wa Israel Netanyahu kulihutubia baraza kuu la umoja
wa mataifa.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
OBAMA NA NETANYAHU.
Kushindwa kutayarisha mkutano kati ya Netanyahu na rais Obama
kumezusha uvumi kuhusu kuongezeka kwa mpasuko kati ya viongozi
hao wawili.
Marekani na washirika wake wameongeza juhudi zao za
kutoa onyo kwa Iran, hata hivyo , muda unafikia tamati kwa
ajili ya kupata suluhisho kuhusiana na mvutano huu.
Netanyahu atahutubia baraza kuu mara baada ya kiongozi wa
Palestina Mahmoud Abbas kuhutubia.
Mwaka jana kiongozi huyo wa
Palestina alikuwa kivutio kikubwa kwa juhudi zake zilizovuta
hisia za kutaka kuwa mwanachama kamili wa umoja wa mataifa,
juhudi ambazo zimezuiwa na Marekani.

0 comments:
Post a Comment