WAZIRI Mkuu wa Somalia amesema kuwa, kundi la kigaidi la ash Shabab
linapoteza nguvu na satua zake kati ya wananchi wa nchi hiyo, huku
likielekea kusambaratika kikamilifu.
Abdiweli Mohamed Ali amesema kuwa,
ana matumaini kwamba mustakbali wa Somalia utakuwa mzuri.
Waziri Mkuu
wa Somalia ameongeza kuwa, mlipuko uliotokea siku chache baada ya
kuapishwa Rais mpya wa Somalia ni ishara ya kudhoofika kundi hilo na
kuelekea kwake ukingoni.
Ameongeza kuwa, Kismayu iliyokuwa kambi na
ngome ya kundi hilo la ash Shabab imeshakuwa mikononi mwa wananchi wa
Somalia baada ya vikosi vya Kenya vikishirikiana na vile vya serikali
kuudhibiti mji huyo wa bandari.
Waziri Mkuu wa Somalia amesema mji wa
bandarini wa Kismayu ni moja kati ya miji iliyokuwa ikitegemewa sana na
kundi hilo katika kujipatia pato la kuendeshea shughuli zake za kigaidi,
na kukombolewa mji huo ni ushindi mkubwa kwa wananchi wa Somalia
0 comments:
Post a Comment