VIONGOZI wa Mali wanajitayarisha na vita, kulikomboa eneo la
kaskazini linalodhibitiwa na makundi ya waasi wa Kiislamu: ni ujumbe
kutoka Bamako katika mkutano wa umoja wa mataifa,licha ya majirani zake
kuwa na shaka.
Tunahisi kuwa jumuiya ya kimataifa inawajibika kwa upande wetu,
ikiwa ni mshikamano na Mali, duru karibu na rais Dioncounda
Traore ililiambia shirika la habari la AFP.
Alikuwa akizungumza katika mkutano siku ya Jumatano mjini New
York, pembezoni mwa mkutano wa hadhara kuu ya umoja wa mataifa,
ambao ulikuwa unalenga kujadili kuhusu mzozo wa eneo la Sahel.
Maafisa wa Mali wanatambua kuwa majirani wa nchi hiyo Algeria
inajaribu kuleta hali ya maelewano na Mauritania na Niger ili
kuzuwia uwekaji wa majeshi ya kigeni nchini Mali, kimesema
chanzo hicho.
Kundi la waasi wa Kiislamu nchini Mali la MUJWA.
LAKINI Ufaransa itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa
baraza la usalama linakutana na azimio linaloidhinisha kuingilia
kati linapatikana, ameongeza afisa huyo.
Raia wanaunga mkono
Mjini Bamako , "watu hawaulizi tena lini vita vitaanza ?, lakini
vipi tunaweza kuweka pamoja masharti muhimu ya kuanzisha vita.
Kwetu
sisi, uingiliaji kati hauko mbali sana, unatayarishwa, chanzo hicho
kimeeleza.
Madou Diallo, profesa wa sheria za kimataifa katika chuo
kikuu cha mjini Bamako, jibu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa
limepunguka makali na la kujizuwia zaidi.
Tunafahamu mapendekezo ya kuchukua tahadhari ya hali ya juu ,
kwa upande wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon,
kwasababu vita hivi vinaweza kusababisha maafa ya kiutu, Diallo
amesema.
Mzozo wa Mali umesababisha mzozo wa wakimbizi.
Lakini wananchi wa Mali kwa jumla inapendelea hatua ya
kuingilia kati upande wa kaskazini, ameongeza. "Hicho ndio
kinasikika mitaani".
Magazeti yako upande gani?
Magazeti nchini Mali hata hivyo yalijishughulisha na masuala mengine.
Hawakutoa umuhimu katika vichwa vya habari katika mjadala
unaoendelea katika umoja wa mataifa lakini wameelekeza kalamu zao
katika mapambano nchini Mali baina ya makundi hasimu ya jeshi
la polisi ambapo watu wawili wamejeruhiwa.
Ghasia kama hizo ni matokeo ya hali ya wasi wasi ambayo
imekuwapo kwa miezi kadha baada ya mapinduzi ya mwezi Machi
ambayo yamemwondoa madarakani rais Amadou Toumani Toure, ambaye amekuwa
madarakani kwa muda wa miaka kumi.
Rais wa Mali Dioncounda Traore
Jeshi na wanasiasa wanavutana.
Mjini Bamako kuna hali ya wasi wasi sana kati ya wanasiasa na
jeshi, amedokeza Gille Yabi, mwakilishi wa Senegal katika kundi la
uchunguzi wa mizozo la kimataifa, ICG.
Jeshi la Mali ni jeshi la baada ya mapinduzi na linahitaji
kutambuliwa na kupewa jukumu katika mapinduzi hayo, ambapo
linawakilisha ukoo muhimu ndani ya jeshi hilo.
Mazungumzo yamepangwa kufanyika mwezi Oktoba katika mji mkuu wa Mali,
Bamako, ambako wahusika wote, vyama vya siasa, vyama vya kijamii,
makundi ya kidini na jeshi , wanaweza kufikia makubaliano juu ya vipi
kipindi cha mpito cha kisiasa kinaweza kushughulikiwa, kimesema chanzo
hicho cha habari kutoka ofisi ya rais.
Uundwaji wa baraza kuu la taifa umeahirishwa, likiwa na makamu wawili wa rais, mmoja akiwa na jukumu la ulinzi.
0 comments:
Post a Comment