ZAIDI ya wachimbaji migodi elfu moja nchini Afrika Kusini, wanafanya
maandamano kutoka katika mgodi wa Marikana ambako wenzao thelathini na
wanne walipigwa risasi na kuuawa na polisi mwezi jana.
Mazungumzo na wamiliki wa kampuni ya madini ya Lonmin,ambayo ndio mwajiri wao, hayajafanikiwa kutatua mgogoro huu wa mishahara.
Migomo mingi isiyorasmi ya wafanyakazi wa migodi ya dhahabu na Platinum imekumba nchi hiyo katika kile kinachooneka kama changamoto kubwa kwa serikali ya Jacob Zuma.
Mapema wiki hii Takriban wachimba migodi 122 waliachiliwa huru na mahakama nchini humo baada ya kesi ya mauaji dhidi yao kutupiliwa mbal.
Hatua hiyo ilitokea siku moja baada ya wendesha mashtaka kufutilia mbali mashtaka dhidi ya wachimba migodi
270 kufutia shinikizo za uma.
Walifikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya wachimba migodi wenzao 34 waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Wachimba migodi wa kwanza miamoja walitarajiwa kuachiliwa leo wengine wakisubiri kuachiliwa siku ya Alhamisi.
Mazungumzo yanayolenga kusitisha mgomo wa wachimba migodi hao wa mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana, vile vile yalitarajiwa kuanza leo.
Polisi wanadai kuwa walilazimika kuwafyatulia risasi wachimba migodi hao kama hatua ya kujilinda kwani na wao walikuwa wamejihami kwa mapanga wakati wakikabiliana nao.
Mgomo wao ulioitishwa kulalamikia nyongeza ya mishahara pamoja na kutaka chama chao kipya cha wafanyakazi kutambuliwa, ungali unaendelea huku mgodi ukisalia kufungwa kwa wiki tatu sasa.
Lakini imetupilia mbali matakwa yake kuwa ikiwa wafanyakazi hao hawatarejea kazini , watafutwa kazi.
Baada ya ufyatuliaji risasi, viongozi wa mashtaka wa serikali, walitumia kanuni ya enzi ya ubaguzi wa rangi ya kosa la ujumla kuweza kuwafungulia mashtaka wachimba migodi 270 waliokamatwa wakati wa vurugu baada ya mgomo wao kuwalazimisha polisi kuwafyatulia risasi.
Kanuni hiyo ilitumika na walowezi wa kizungu wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi kuwanyanyasa wapinzani wao waafrika weusi.
0 comments:
Post a Comment