BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BINGWA WA MKANDA WA UBO, FRANSIC CHEKA ATUA MORO BAADA YA KUMTANDIKA KALAMA NYILAWILA KWA KO JIJINI DAR ES SALAAM.

 BONDIA FRANCIS CHEKA "SMG" AKIWA NA WAPAMBE NA WALIMU WAKE HUKU WAKIWA WAMESHIKILIA BAADHI YA MIKANDA YA UBINGWA MBALIMBALI WAKATI WAKIWASILI MANISPAA YA MOROGORO BAADA YA KUCHUKUA MKANDA MWINGINE KUFUATIA KUMTANDIKA KALAMA NYILAWILA JIJINI DAR ES SALAAM HIVI KARIBUNI
 CHEKA AKIWA KLABU KWAKE DDC NA BAADHI YA WAPENZI WA MCHEZO W NGUMI WAKATI WA MAKOPEZI YAKO.
SMG AKIZNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) KLABUNI KWAO DDC KATA YA KINGO MANISPAA YA MOROGORO.

BINGWA wa UBO, Francis Cheka "SMG" ameitaka Serikali kuwekeza kwa vitendo katika michezo ukiwamo mchezo wa ngumi ili kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi nchini.

Cheka alisema hayo baada ya kuwasili mjini Morogoro akitokea Dar es Salaam alipofanikiwa kunyakua ubingwa wa UBO baada ya kumchapa Karama Nyilawila kwa TKO raundi ya sita.

Alisema inasikitisha kuona Serikali haijali kazi za vijana wanazofanya kila siku wakati ndiyo ajira yao hasa kwenye wa michezo.

Vijana wanajitahidi kujiongezea kipato kiugumu kweli, lakini Serikali imetelekeza michezo na kuegemea zaidi kwenye soka, wakati ni wazi kwamba wote hatuwezi kuwa wacheza mpira," alisema Cheka.

Kwa upande wa kocha Abdalah Saleh 'Komandoíanayemnoa Cheka yeye aliwataka mapromota wa mchezo huo nchini kubadili mfumo kwa kuwaita mabondia kutoka nje kutokana na Cheka kuwa kiwango cha juu cha kupigana hivi sasa.

Unajua Cheka amekua, kuendelea kumkutanisha na mabondia hawa nchini ni kumchosha na inaweza kusababisha madharaÖniwashauri mapromota kuwaleta mabondia wenye uwezo mkubwa hasa kutoka njeÖkwanza itamwongezea ujuzi zaidi na kiwango kitaongezeka,îalisisitiza Komando.

Wakati huohuo; Baada ya kupigwa wa TKO raundi ya sita, bondia Karama Nyilawila ameporomoka kwa nafasi 26 zaidi kwenye viwango vya ngumi vya dunia huku mbabe wake, Francis Cheka akipanda kwa nafasi 17.

Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, Nyilawila ameporomoka hadi nafasi ya 99 kutoka 73 aliyokuwa mwezi uliopita akiwa na pointi 42 kulinganisha na 58 za awali.

Hata hivyo Cheka amezidi kuchanja mbuga hadi nafasi ya 27 kutoka 44 aliyokuwa awali na kupata pointi 139 kulinganisha na 90 za mwezi uliopita.

Kipigo alichopewa Nyilawila mwishoni mwa wiki katika pambano la ubingwa wa UBO dhidi ya Cheka ndicho kimechangia kumshusha kwenye viwango vya dunia licha ya kuendelea kung'ang'ania namba mbili ya ubora hapa nchini.

Mtandano huo ulibainisha kuwa bondia namba tatu hapa nchini, Mada Maugo yuko nafasi ya 123 duniani huku Mtanzania Dickson Mwakisopile akikamata mkia bila pointi akiwa nafasi ya 914.

Rashid Matumla amepanda kwa nafasi moja kutoka ya 10 aliyokuwa awali hadi ya 9 kwenye viwango vya Tanzania huku Japhet Kaseba akiondolewa kwenye viwango hivyo.

Maneno Oswald, Said Mbelwa, Benson Mwakyembe, Kanda Kabongo na George Dimoso walikamata nafasi ya nne hadi ya nane.
Juma Mtanda, Morogoro na Imani Makongoro Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: