SERIKALI ya Afghanistan inaweza kuanguka baada vikosi vya NATO
kuondoka nchini humo 2014, hasa iwapo uchaguzi wa urais utahusisha
udanganyifu, Kundi la Kimataifa linaloshughulikia mizozo (ICG) limesema.
Nchi ya Afghanistan inaweza kuanguka baada vikosi vya NATO kuondoka
nchini humo mwaka 2014, hasa iwapo zoezi la uchaguzi litahusisha
vitendo vya udanganyifu, Kundi la Kimataifa linaloshughulikia mizozo
limesema katika taarifa yake.
Mchambuzi wa ngazi ya juu wa kundi hilo nchini Afghanistan, Candace
Rondeaux amesema kuna mashaka makubwa kwamba serikali ya Afghanistan
inaweza kuporomoka kwa kuondoka kwa majeshi ya Jeshi la NATO.
Ameongeza
kusema kuwa fursa ya marekebi &sho nayo inayoyoma kwa haraka.
Askari wa ulinzi wakiwa katika doria mjini Kabul.
TAARIFA HIYO ILIYOPEWA JINA LA AFGHANISTAN:
Barabara ndefu na ngumu hadi
kipindi cha mpito kuelekea 2014, inasema taifa hilo linaelekea kuwa na
uchaguzi uliojaa visa vya udanganyifu, baada ya kuendesha uchaguzi wa
urais na wabunge wa mwaka 2009 na 2010 uliogubikwa na vurugu za kila
aina.
Iwapo machafuko yatatokea tena katika uchaguzi wa urais ujao
Afghanistan, matumaini finyu yaliyopo ya amani kurejea tena nchini humo
yatapotea kabisa, baada ya serikali hiyo kuchukua jukumu zima la ulinzi
wake kutoka kwa vikosi vya Jeshi la NATO, vinavyoongozwa na Marekani.
Hayo ni kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Kundi la Kimataifa
linaloshughulikia mizozo ICG, lenye makao yake makuu mjini Brussels,
Ubelgiji.
Ushirika huo ambao umepigana vita kwa miezi 11 sasa dhidi ya wanamgambo
wa Taliban, unapunguza idadi ya askari wake kutoka 130,000 ambapo mpaka
kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 askari wote wanatakiwa kuwa
wamekwisharejea nyumbani.
Watoto kama huwa huathirika na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Kundi la Taliban.
KWA mujibu wa maelezo ya mchambuzi huyo Rondeaux, polisi wamelemewa
na aghalab hushambuliwa na wapiganaji hao wa Taliban. Rais Hamid Karzai
na bunge lake wameshindwa pia kuchukua hatua thabiti za kuandaa zoezi la
uchaguzi lililo huru na la haki.
Karzai anachojali ni kuwa na ushawishi tu uongozini: Candace Rondoeaux.
Aidha, mchambuzi huyu anasema Karzai anaonekana kujali zaidi kuendeleza
nguvu yake badala ya kuhakikisha Afghanistan inakuwa na mfumo imara wa
siasa na utulivu.
Ingawaje amesema bayana kuwa ataondoka madarakani
mwaka miaka miwili ijayo, kama katiba ya nchi inavyodai, lakini kuna
hofu kuwa anaweza kusababisha hila katika uchaguzi huo ili kumweka mtu
wake wa karibu madarakani, bila shaka mmoja wa kaka zake.
Wakati huohuo, mawaziri wa ulinzi wa NATO watapitisha mkakati mpana wa
mafunzo yatakayoendeshwa Afghanistan baada ya kuondoka kwa majeshi ya
NATO, wakati ambapo machafuko yanaendelea kutokea nchini humo na kuzua
maswali mengi juu ya usalama wa nchi hiyo.
Mawaziri hao watakaokutana kesho na Jumatano mjini Brussels, yalipo
makao makuu ya umoja huo, wanatazamiwa kuidhinisha mpango huo unaolenga
kutoa mafunzo, ushauri na msaada kwa majeshi ya ulinzi ya Afghanistan,
yatakayobeba jukumu la kulinda nchi hiyo kuanzia mwihoni mwa mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment