BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

OKTOBA SABA: NI SIKU YA MAADHIMISHO YA VITA AFGHANISTAN.

 http://gdb.voanews.eu/D94E2214-E877-481D-AB7C-8794E45AA763_w443_r1.jpg
 Askari wa Marekani nchini Afghanistan.
 http://gdb.voanews.eu/58504012-E273-4092-9C61-F7D5A2CC82E6_w640_r1_s.jpg
 Mwanajeshi wa Marekani akipiga doria kwenye kituo cha polisi baada ya shambulio la wanaharakati. June 19, 2012.

OKTOBA saba ni maadhimisho ya miaka 11 ya kuanza vita vilivyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.

Vimedumu kwa muda mrefu zaidi kuliko vita vingine katika historia ya Marekani. Zaidi ya wanajeshi 3000 wa kimataifa wamekufa katika vita ikiwemo wamarekani 2000.


Raia wa Afghanistan pia wamekufa katika vita hivi. Vita vilichochewa na mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani Septemba 11 mwaka 2001 .


Chini ya mwezi mmoja baadae vikosi vya jeshi la Marekani viliingia katika ardhi ya  Afghanistan kushambulia kundi la wanamgambo wa Al- qaida na serikali ya utawala wa Taliban ambayo iliongoza mtandao wa kigaidi.

 Taliban iliondolewa haraka. 
Lakini wanamgambo waasi wameongeza nguvu kwa miaka kadhaa. Marekani na vikosi vya kimataifa vya pamoja vimekabiliwa na mfululizo wa mashambulizi yanayojulikana kama “mashambulizi ya ndani”  yanayofanywa dhidi ya  jeshi la muungano wa nchi za magharibi  na wanajeshi na polisi wa Afghanistan.

Majeshi ya pamoja yameanza kujiondoa nchini humo huku majeshi yote ya kigeni wamepanga kkuondoka ifikapo mwaka 2014.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: