MWENYEKITI MPYA WA CCM MKOA WA MOROGORO, INNOCENT KALOGERIS AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI AKIPONGEZWA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO KATIKA UKUMBI WA MAGADU MESS BAADA YA KUIBUKA MSHINDI KATIKA UCHAGUZI WA NAFASI HIYO YA MWENYEKITI KWA KUPATA KURA 779 AKIWASHINDA MWENYEKITI ALIYEMALIZA MUDA WAKE MHANDISHI PETROL KINGO ALIYEPATA KURA 291 NA BI HENAYA DIMOSO KURA 86 JANA USIKU.
MWENYEKITI MPYA WA CCM MOROGORO INNOCENT KALOGERIS AKITAFARI JAMBO MARA BAADA YA KUSHINDA NAFASI HIYO KWA KUWASHINDA WAPINZANI WAKE WAWILI KATIKA KICHANG'ANYIRO CHA NAFASI HIYO.
RAHA YA USHINDI NDIYO HUU, MWENYEKITI HUYU AKIFURAHIA USHINDI NA WAJUMBE WA MKUTANO KUU WA CHAMA HICHO BAADA YA KUSHINDA.
MWENYEKITI MPYA WA CCM MOROGORO INNOCENT KALOGERIS AKITOA SHUKURANI KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU HUO, KUSHOTO NI MSIMAMIZI MKUU WA UCHAGUZI HUO MAMA YETU ZAKIA MEGHJI NA KULIA NI KATIBU WA CCM MKOA MOROGORO SIXTUS MAPUNDA.
MSIMAMIZI MKUU WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA MOROGORO ZAKIA MEGHJI AKISOMA MATOKEO YA UCHAGUZI WA NAFASI MBALIMBALI KATIKA UCHAGUZI HUO.
MWENYEKITI ALIYEMALIZA MUDA WAKE MHANDISI PETROL KINGO AKISIKILIZA MOJA YA MASWALI MARA BAADA YA KUOMBA KURA KATIKA NAFASI HIYO AKIOMBA WAJUMBE WAMREJESHE KWENYE NAFASI HIYO.
MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MOROGORO BI HENAYA DIMOSO AKIOMBA KURA KWA WAJUMBE KATIKA MKUTANO HUO.
MWENYEKITI WA KAMATI YA USALAMA MKOA WA MOROGORO AMBAYE NI MKUU WA MKOA HUO, JOEL BENDERA AKIZUNGUMZA JAMBO KABLA YA KUANZA KWA UPIGAJI WA KURA WA KUCHAGUA VIONGOZI MBALIMBALI, WA PILI NI KATIBU WA CCM MKOA WA MOROGO SIXTUS MAPUNDA, MHANDISI PETROL KINGO NA MSIMAMIZI MKUU WA UCHAGUZI HUO, ZAKIA MEGHJI.
MKUU WA MKOA WA MOROGORO MSTAAFU, STEVEN MASHISHNGA (KATIKATI) AKIWA NA MKUU WA WILAYA YA MOROGORO SAIDI AMANZI KULIA NA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO ABDULLAZIZ ABOOD KUSHOTO WAKIFUATILIA MATUKIO KATIKA MKUTANO HUO.
SEHEMU YA UMATI WA WAJUMBE WA MKUTANO HUO KUTOKA WILAYA SITA ZINAZOUNDA MKOA WA MOROGORO, KILOSA, KILOMBERO, MOROGORO, GAIRO, ULANGA, MVOMERO NA MOROGORO VIJIJINI WAKIFUATILIA KWA KARIBU MATUKIO MBALIMBALI YALIYOKUWA YAKIJITOKEZA.
0 comments:
Post a Comment