BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI YATAKA RIPOTI ARV BANDIA KUTINGA BUNGENI

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.
KAMATI ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi imeishauri serikali kutoa tamko la kuelezea ni hatua gani inaendelea kuchukua baada ya kusimamisha kazi baadhi ya viongozi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kufuatia kuwepo kwa dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi( ARV) katika kikao cha Bunge kitakachoanza mwishoni mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Lediana Mng’ong’o wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam kuhusu kuwepo kwa dawa hizo.

“Sisi tungependa kuishauri serikali kuendelea kufuatilia na hatua za kisheria pale itakapobaini katika uchunguzi huo ili tatizo hili lisiendelee kutokea,” alisema Lediana ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Iringa.

Aliongeza kuwa wanaishauri Mamlaka cha Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na wawakilishi katika kanda mbalimbali ili kuweza kudhibiti tatizo la kuwepo kwa dawa bandia.

Aidha kamati hiyo imelaani kampuni ambayo imeingiza dawa feki na imetaka hatua za kisheria zichukuliwe.

Kamati hiyo imewataka watu wanaotumia dawa hizo kutoziacha , bali waendelee kuzitumia kwa kuwa dawa zote si feki na pia zipo za kutosha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: