BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI YAATHIMISHA KIMATAIFA.

 Watoto wa kike wa Yemen wakihudhuria shule katika siku yao ya kwanza kuadhimishwa kimataifa.http://gdb.voanews.eu/9A04E9DF-80AC-417C-8CF1-B268027C7EEE_w443_r1.jpg 

 Ripoti mpya inaonesha hali duni ya wasichana wasioelimishwa huku Umoja wa Mataifa ukiadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike Octoba 11.

Shirika la Plan International linasema huku idadi ya wasichana na wavulana wanaojiunga na shule duniani ikielekea kuwa sawa katika shule za msingi, wasichana wengi hata hivyo hawakamilishi masomo yao.


Shirika la maendeleo ya wasichana linasema wasichana milioni 39 wa kati ya umri wa miaka 11 hadi 15 hawamalizi masomo yao katika shule za msingi.


Mkurugenzi wa shirika la Plan Internatinal Nigel Chapman anasema mara nyingi wasichana wanavyokua familia zao zinawaomba kuchangia kiuchumi na kwa hiyo wengi wanalazimika kuacha masomo yao shuleni.


Anasema tatizo hili ni sugu zaidi barani Afrika. Aidha shirika hilo pia inasema matatizo mengine yanayochangia wasichana kuacha shule ni pamoja na ndoa za mapema na kupata mimba wakiwa bado wadogo.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: