LOWASSA KUSHOTO NA SITTA KULIA. |
NI MWANZA, SHINYANGA, ARUSHA, MGOMBEA APIGWA
KAMBI
ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, imeendelea kuzidi kujiimarisha
katika uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya
wagombea wanaomuunga mkono kuzidi kupata ushindi.Katika chaguzi
zilizokwishafanyika katika ngazi ya wilaya na mikoa, wagombea wengi wa
Umoja wa Vijana (UVCCM), Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Wazazi
waliokuwa katika kambi nyingine ndani ya chama hicho wameshindwa.
Hata
hivyo, katika uchaguzi wa UVCCM mkoa ambao ulifanyika jana katika mikoa
kadhaa nchini inaonyesha kuwa kambi hiyo ya Lowassa inayoratibiwa na
Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa, Beno Malisa na Hussein Bashe
wagombea wake wengi wameibuka na ushindi.
Habari zilizopatikana
zinaeleza kuwa Kambi ya Kada wa CCM, Bernard Membe ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Nje ya Nchi inaongozwa na Ridhwan Kikwete ambaye ni Mjumbe
wa Utekelezaji wa Baraza la Vijana wa chama hicho, ambaye kwa sasa
amekuwa akipita mikoani kuongezea nguvu kambi yake.
Mkoani Arusha
chaguzi hizo zilimalizika jana kwa wilaya nne za Mkoa wa Arusha,
isipokuwa wilaya moja ya Longido, ambako uchaguzi unatarajiwa kurejewa
katika nafasi ya NEC.
Katika Wilaya ya Ngorongoro, Mbunge wa
jimbo hilo, Saning’o Ole Telele alitangazwa kuwa mshindi wa NEC baada ya
kupata kura 457 dhidi ya Mathew Nasay ambaye alipata kura 323 na
Ibrahim Sakayi kushinda nafasi ya mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo kwa
kura 517 na kumbwaga aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Metui Ole
Shaudo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji wa Ngorongoro.
Longido, Laizer akwama
Licha
ya Mbunge wa Jimbo la Longido, Lekule Laizer kutangaza kutogombea
ubunge katika uchaguzi ujao na kuomba achaguliwe kuwa mjumbe wa NEC
kupitia Longido, alishindwa kupata nafasi hiyo.
Kukwama Laizer
kuwa mjumbe wa NEC , kulitokana na kushindwa kupata nusu ya kura,
hatua ambayo iliibua malumbano kadhaa licha ya kuongoza katika kura.
Msimamizi
wa uchaguzi huo, George Kijazi, alitangaza matokeo ya uchaguzi huo
usiku wa manane, kuwa Laizer amepata kura 417 na Peter Lemshau kura 381
huku mgombea mwingine akipata kura 58.
Katika uchaguzi wa nafasi
ya mwenyekiti, Makoro Sauni alichaguliwa baada ya kupata kura 368,
Emanuel Laizer alipata kura 182 na Kishiri Ole alipata kura 358.
Kaaya atupwa NEC
Katika
Wilaya ya Arumeru, ambapo kulikuwa na upinzani mkali, Elishilia Kaaya
ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha,(AICC), alishindwa nafasi ya NEC na Julius Mungure.
Katika
uchaguzi huo, Kaaya ambaye alikuwa mjumbe wa NEC wa Mkoa wa Arusha,
alipata kura 215, Mungure kura 535 Meja mstaafu Irikael Mbise alipata
kura 51.
Katika uchaguzi huo, Furahia Nderea alichaguliwa
kuwa mwenyekiti wa wilaya kwa kupata kura 430, ambapo Christopher
Pallangyo alipata kura 257 na Severa Minja alipata kura 148.
Lowassa ang’ara Monduli
Kwa
upande wake Lowassa alishinda katika jimbo lake la Monduli kwa kupata
kura nyingi dhidi ya Dk Salash Toure ambaye pia anagombea nafasi ya
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha.
Dk Toure pia alishindwa wakati
wa kuwania kuteuliwa kuwania ubunge katika jimbo hilo katika kura za
maoni ndani ya CCM na safari hii pia anatarajiwa kuchuana na Mwenyekiti
wa sasa wa CCM, Onesmo Nangole ambaye ni mfuasi mkubwa wa kambi ya
Lowassa.
Mwalusamba na Awaki
Katika wilaya
za Karatu na Arusha napo kumefanyika mabadiliko makubwa baada ya Godfrey
Mwalusamba kuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC akiwakilisha Wilaya ya
Arusha, huku Daniel Awaki akichaguliwa kuwa mjumbe wa NEC wa Wilaya ya
Karatu.
Katika uchaguzi huo, viongozi kadhaa waliokuwapo
wameshindwa na mabadiliko makubwa yametokea katika Wilaya ya Arusha,
ambapo Jubilate Kileo aliyekuwa mwenyekiti pamoja na kamati yake nzima
ya siasa walishindwa.
Dk Wilfred Soileli ndiye alichaguliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha.
Vurugu Shinyanga
Mgombea
Uenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani Shinyanga, Luhende Richard
na mpambe wake juzi walivamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana, huku
makada wakongwe wa chama hicho wakigeuka mabubu kuzungumzia kushindwa
kwao.
Vurugu hizo zinazodaiwa kufanywa na kundi linalompinga
Richard zilitokea juzi saa 2.00 usiku, katika tukio ambalo linadaiwa
kupewa baraka na wabunge wawili wa chama hicho (majina tunayo), pamoja
na mbunge mmoja wa upinzani.
Richard na mpambe wake aliyetajwa
kwa jina moja la Paschal walitoroshwa eneo hilo na kupelekwa Shinyanga
mjini ili kuwaepusha na kipigo.
Ng’enda aibuka
Kada
maarufu Kilumbe Ng’enda ameibuka mshindi kwa kura 434 kati ya 742
zilizopigwa na kuwamwaga wapinzani wake wawili katika kinyang’anyiro cha
kuwania nafasi ya kiti cha ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kigoma
Mjini.
Aliyemfuatia katika nafasi ya pili ni Anthon Mpozemenya
aliyejipatia kura 272 huku Athuman Kitimba akiambulia nafasi ya tatu kwa
kura 26 ambapo kura 10 ziliharibika.
Katika wilaya hiyo yenye kata 21halmashauri ilikuwa imepitisha majina hayo matatu ili kumpata mwakilishi katika ngazi ya taifa.
Chilolo awa shujaa
Diana Mkumbo Chilolo, ametetea kwa kishindo nafasi yake ya Mwenyekiti UWT (CCM) Mkoa wa Singida, baada ya kupata kura 431 dhidi ya 451 zilizopigwa.
Kwa ushindi huo, Chilolo ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu mkoani hapa, aliwaacha kwa mbali wapinzani wake Pendo Kone aliyepata kura 11 na mwalimu Sundi Samike aliyeambulia nane.
Msimamizi wa mkutano huo mkuu wa uchaguzi, Dk Parseko Kone, alimtangaza Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Fatuma Towfiq kuwa amechaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu taifa UWT.
Alisema mfanyakazi wa Tanroads mkoani Singida, Sara Mkumbo, amemgaragaza vibaya mpinzani wa Mwajuma Shaa kwa kura 247 dhidi ya 153.
Aliwataja washindi wa Baraza la UWT kutoka Wilaya ya Singida Vijijini kuwa ni Halima Kundya na Debora Andrew.
Alisema kutoka Wilaya ya Ikungi ni Mariamu Limu na Tatu Dahani; Wilaya ya Iramba, Monica Samwel na Elimaba Lula, Wilaya ya Mkalama, Mariamu Kahola na Helena Kitila, Manispaa Singida ni Aisha Matembe na Sara Mkumbo. Wilaya ya Manyoni ni Magreth Mlewa na Rehema Chizumwa.
Naye Hadija Nyuha ameshinda nafasi ya uwakilishi wa Jumuiya ya Wazazi kwenye Mkutano Mkuu wa UWT na mwakilishi wa UVCCM ni Janet Mughwai. Jane Kishari anakuwa mjumbe kwenye mkutano mkuu wa CCM mkoa.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ashinda
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumaa Hamidu Awesso (25) ameshinda nafasi ya ujumbe wa NEC Wilaya ya Pangani kwa kura 377 na kuwabwaga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Salim Sinani aliyepata kura 80 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Pangani Rajabu Issah aliyepata kura 97.
Naye Julius Semwaiko alimtaja Hamisi Mnegero kuwa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya kwa kura 262 akiwabwaga Hamisi Makumulo aliyepata kura 226 na James Kasongo
Mnangwa kura 51.
Walioshinda nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kwa mujibu wa matokeo yaliyosomwa na Guledi ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Hafsa Mtasiwa kura 325; Diwani wa Kata ya Pangani Magharibi, John Semnkande (252), Fatma Selemani Chee (282) Habiba Abdallah (173) na Elizabeth Mfugale (272).
Aisha Kigoda aibuka
Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Aisha Kigoda amepita bila kupingwa katika uchaguzi wa nafasi ya Uwenyekiti wa UWT Mkoa Tanga kutokana na mgombea mwenzake kujitoa.
Imeandikwa na Gasper Andrew, Singida, Mussa Juma, Arusha, Burhani Yakub, Pangani, Mussa Juma, Loliondo, Raisa Said, Tanga, Shija Felician, Shinyanga

0 comments:
Post a Comment