MADAKTARI wanaofanya kazi kwenye hospitali za serikali huko
Misri wameanza mgomo wao wa upande mmoja huku wakijizuia kutoa huduma
zisizo za dharura kwa wagonjwa wakilalamikia huduma mbovu za afya na
mishahara duni.
Khairy Abdul Dayem Mkuu wa Jumuiya ya Madaktari alisema
hapo jana huko Cairo mji mkuu wa Misri kuwa mgomo huo utazijumuisha
hospitali za serikali zisizopungua 540 kiwango ambacho ni sawa na
asilimia 40 ya huduma za afya zinazotolewa kwa raia kote nchini humo.
Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za serikali wanalipwa
mshahara wa dola 46 kwa mwezi huku wengi wao wakilazimika kufanya kazi
kwenye hospitali za watu binafsi au zahanati nyinginezo kwa masaa mengi
ili kuongeza kipato chao.
Mwanachama mmoja wa Jumuiya ya Madaktari wa
Misri amenukuliwa akisema kuwa na hapa ninmnukuu, "hospitali za serikali
nchini Misri zimejaa wagonjwa na hazitoi huduma inayotakikana kwa
wagonjwa kutokana na uhaba wa fedha," mwisho wa kunukuu.
0 comments:
Post a Comment