Katibu Mkuu Mtendaji wa Shimiwi, Ramadhan Sululu
(mwenye kofia nyeupe) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mratibu
wa Masoko kutoka taasisi ya fedha ya Platinum Credit Ltd, Richard Rwegesila
wakati Katibu huyo akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo zinavyotumika kwa uongozi wa juu
wa shirikisho hilo na waamuzi vyenye thamani ya sh1.5Mil katika hafla fupi iliyofanyika
uwanja wa Jamhuri, kulia ni Mtunza fedha wa Shimiwi, Frank Kibona na kushoto ni
mkuu wa kitengo cha mauzo taasisi hiyo ya fedha,Ferdinand Kambanyumba.
Mwanariadha wa kutoka Ikulu Sport Club Saleh Ahmadi akimaliza mbio za mita 100 na kushika nafasi ya kwanza akitumia sekunde 11:58 wakati wa mbio hizo kwa wanaume katika uwanja wa Jamhuri.
Akinadada nao wakichukua katika mbio za mita 200 katika uwanja huo.
Amina Mavenero wa idara ya Uhamiaji (Mbele) akimaliza mbio za wazee kwa kutumia sekunde 17:34 kwa upande wa akina mama.
Hii ilikuwa moja ya vijana wakionyesha kazi kwa kufukuza upepo katika hatua za awali za mbio za mita 100 na jamaa ndiyo alishika nafasi ya kwanza.
Mbio za kupokezana vijiti zilianza hivi kabla ya kupataikana mshindi.
Huu ndiyo mchezo wa kurusha tufe wakati wa mashindano hayo ya Shimiwi 2012.
JUMLA ya timu 32 za michezo mitatu
tofauti zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kufanya vizuri
katika hatua ya mzunguko wa pili wa 16 bora katika mashindano yanayoendelea ya
shirikisho la Michezo ya Idara za Serikali, Wizara na Ofisi za Wakuu wa Mikoa
(SHIMIWI) katika viwanja vine katika Manispaa ya Morogoro.
Kwa upande wa michezo hiyo
inajumuisha soka, netiboli kamba wanaume na wanawake huku kila mchezo ikibakiwa na timu nane wakati nane nyingine zikiaga
mashindano katika hatua hiyo ya mtoano 16 bora.
Katibu wa kamati ya ufundi katika
shirikisho hilo (SHIMIWI), Joyce Benjamin alisema jumla ya timu 32 zimefuzu
kuingia katika hatua ya robo fainali baada ya kushinda michezo ya hatua ya
mzungumko wa pili wa 16 bora katika michezo ya mtoano.
Benjami alitaja matokeo ya michezo
hiyo akianzia na mchezo wa soka kuwa Uhamiaji iliitandika Bunge kwa bao 3-0,
Kilomo nayo ikiilaza Afya kwa idadi kama hiyo ya bao 3-0 katika michezo
iliyofanyika kwenye uwanja wa chuo cha Ujenzi Morogoro.
Ukaguzi ilijihakikishia kuchezo robo
fainali baada ya Mambo ya Nje kwa bao1-0 huku Ikulu ilinda kwa changamoto ya
mikwaju ya penalti 5-4 na Mahakama baada ya kuisha dakika za kawaida bila
kufungana katika uwanja wa chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) wakati GST
ikiitambia Hazina kwa kuifunga bao 2-0 huku Maji nayo ikiiga mashindano hayo
kwa kukubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Elimu katika uwanja wa Morogoro Sekondari.
Ras Morogoro ilikubali kipigo cha
bao 1-0 na kuaga michuano hiyo kutoka
kwa Ras Pwani wakati Tamisemi iliitandamiza kwa bao 3-0 Mifugo na Uvuvi katika
mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri.
Benjamin alitaja timu kwa upande wa
mchezo wa netiboli zilizofanikiwa kutinga robo fainali kuwa mabingwa watetezi
Ikulu ikiifunga Mifugo na Uvuvi kwa idadi ya vikapu 24-14, Madini iliifungasha
virango Kilimo kwa vikapu 32-25, Uhamiaji ikiifunga Uchuguzi kwa vikapu 31-19,
na Ras Dar es Salaam ikiondolewa katika hatua hiyo na Ras Pwani michezo
iliyochezwa katika uwanja namba moja wa Jamhuri.
Timu nyingine zilizofuzu kwenye
hatua hiyo ni Ardhi iliisambaratisha Utumishi kwa vikapu 22, Hazina ikipoteza
mchezo dhidi ya Ukaguzi kwa kukubali kufungwa vikapu 36-19, Elimu nayo ikiaga
katika hatua hiyo ya mtoano kwa kupoteza kwa vikapu 21-26 dhidi ya Mahakama na
Afya ikaifunga Tamisemi kwa vikapu 25-21.
Katika mchezo wa kamba wanaume timu
zilitinga robo fainali ni Maliasili ikiishinda Ujenzi kwa kuwavuta 2-0, Hazina
ikiiondoa Mahakama 2-0, Waziri Mkuu ikiitoa Haki 2-0, Utumishi ikishindwa kwa
Afya 2-0, Mipango ikiondolewa na Uchuguzi, Bunge ikipoteza dhidi ya Kilimo,
Mahakama ikishinda kwa shidi kwa kuiondoa Uhamiaji 2-1 na Ikulu ikishinda 2-0
kwa Mambo ya Ndani.
Kwa upande wa wanawake mchezo huo wa
kuvuta kamba Tamisemi iliiondoa Ujenzi 2-0, Ras Iringa ikiitambia Makamu wa
Rais 2-0, Waziri Mkuu ikishindwa kuvurukuta mbele ya Mahakama kwa kupteza 2-0,
Afya ikipata ushindi mbele ya Tume Sheria 2-0, Uchuguzi ikipata ushindi kwa Ras
Kagera, GST ikishindwa kutamba kwa Hazima na kulala 2-0, Mifugo na Uvuvi
ikipoteza kwa Polisi na Mambo ya Ndani ikashindwa kutamba mbele ya Ikulu kwa
kupoteza 2-0.
Mchezo hiyo imeendelea leo (jana)
kwa michezo ya riadha kuanzia mita 100 hadi 800 na wazee mita 100, tufe
wakati kesho (leo) inaanza michezo ya robo fainali soka, netiboli, kamba na
karata katika uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 2 asubuhi.
0 comments:
Post a Comment