Wanajeshi wa Kenya
JESHI la Kenya linasema majeshi yake yameingia kwenye mji wa Kismayo
nchini Somalia katika operesheni ya kuuchukua tena mji huo kutoka kwa
wanamgambo wa al-Shabab wenye uhusiano na al-Qaida.Msemaji wa jeshi la Kenya, Kanali Cyrus Oguna anasema shambulizi la mapema Ijumaa lilijumuisha majeshi yote ya majini na ya anga yakishirikiana na wanajeshi wa Umoja wa Afrika na ya serikali ya Somalia.
Oguna alisema mji huo ulitekwa "bila upinzani mkubwa", hata hivyo mashahidi na majeshi ya al-Shabab wanasema mapigano yanaendelea ndani na kuzunguka mji huo.
Bandari ya Kismayo, Somalia
Mwanzoni mwa wiki hii Kenya ilisema jeshi lake lilifanya mashambulizi ya
anga kwenye maeneo muhimu ya waasi huko Kismayo. Wanamgambo wa
al-Shabab wanatumia bandari ya mji huo kuingiza silaha na vifaa vingine
ili kuwasaidia waasi wenzao kupambana dhidi ya serikali.
Mji wa Kismayo
Kundi hilo la uasi linataka kuweka utumiaji wa sheria kali ya ki-islam
kote nchini Somalia. Kundi hilo liliwahi kudhibiti eneo la kusini na
kati kati mwa Somalia, lakini limepoteza mamlaka yake yote na kwenda kwa
majeshi yanayounga mkono serikali tangu yalipofanya shambulizi moja
kubwa la kujilinda mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment