BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKAMU WA RAIS ZANZABAR AONGOZA WANANCHI KATIKA MAADHIMISHO YA UMOJA YA MATAIFA YA 67.

http://mkr1znz.files.wordpress.com/2012/10/un2.jpg
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya 67 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.

UMOJA wa Mataifa umeahidi kukuza na kuimarisha mashirikiano yake na Zanzibar katika kuendeleza miradi mbali mbali ya kijamii, kiuchumi na maendeleo.

Mwakilishi mkaazi wa Umoja huo nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou ameeleza hayo katika hafla maalum ya kuadhimisha miaka 67 ya Umoja huo iliyofanyika hoteli ya Serena mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amemuhakikishia mwakilishi huyo kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na umoja huo katika kuhakikisha kuwa unatimiza malengo yake ya kuimarisha miradi ya maendeleo hapa Zanzibar.

Amesema umoja huo umekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono miradi ya kijamii ikiwemo ile ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo imekuwa ikiisaidia Zanzibar kuweza kukabiliana na athari za janga hilo la kimataifa.

Amesema ofisi yake chini ya shirika la umoja huo imekuwa ikitekeleza mradi wa mabadiliko ya tabia nchi ambao umeanza kuonesha mafanikio mazuri, na kwamba itasimamia mradi huo kikamilifu ili uwe kigezo cha mafanikio kwa miradi mengine iliyo chini ya umoja huo.

Hata hivyo amesema wakati umoja huo ukiadhimisha miaka 67 tangu kuanzishwa kwake, bado una kazi kubwa ya kuimarisha ustawi wa jamii, ili kufikia maana halisi ya ujumbe wa mwaka huu ambao ni kubadilisha hali ya maisha ya wananchi kwa kukuza maendeleo yao.

Amesema mafanikio hayo hayatofikiwa ikiwa umoja huo hautachukua juhudi za makusudi za kujenga mazingira bora ya kiusalama na amani miongoni mwa mataifa mbali mbali duniani ambayo ndio nyenzo ya kupatikana maendeleo endelevu.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohd Aboud Mohd ameupongeza umoja huo kwa kuanzisha tawi lake hapa Zanzibar, ambalo limerahisisha shughuli za umoja huo kwa wananchi katika maeneo tofauti likiwemo kukuza utawala bora.

Amesema jumuiya hiyo ya kimataifa imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kutunza amani duniani licha ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika baadhi ya nchi, sambamba na kuwatunza watu wasiokuwa na hatia walioathirika kwa hali moja au nyengine kutokana na machafuko.

Habari na Hassan Hamad, picha Salmin Said, OMKR
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: