
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akijari kuwasha moja ya pikipiki tano alizotoa kwa chama cha waendesha pikipiki Manispaa ya Morogoro zenye thamani ya sh800,000 wakati wa uzinduzi wa ofisi na katiba ya chama hicho katika mtaa wa Simu kata ya Mjipya mkoani hapa, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho, Anamwikira Massawe na mwenye kofia ni katibu Juma Bega. 

Mhe Abood akimkabidhi mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki Manispaa ya Morogoro ], Anamwikira Massawe kadi ya pikipiki katika sherehe hizo, na kushoto ni katbu wa chama hicho Juma Bega.
Mhe akikata utepe ikiwa ishara ya ufunguzi wa ofisi hiyo.
Akizungumza na wanachama wa chama cha waendesha pikipiki muda mfupi baada ya uzinduzi huo.
Sehemu ya wageni waalikwa akiwemo mwandishi wa gazeti la Mwananchi Lilian Lucas kulia akichukua dondoo kwa ajili ya habari.
Wanachama wa chama hicho wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika uzinduzi huo.
Moja ya pikipiki ikiwa imebebwa juu mara baada ya kutelemshwa kutoka kwenye gari (halipo pichani) kabla ya kuanza shughuli za uzinduzi wa chama hicho na katiba.
Na Lilian Lucas,Morogo
WAENDESHA pikipiki
maarufu kama bodaboda katika manispaa ya Morogoro wametakiwa kutokuwa chanzo
cha vifo vya watu na badala yake kuwa waadilifu na wenye kutii sheria za
usalama barabarani.
Mbunge wa jimbo la
Morogoro mjini Abdullah Azizi Abood alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi
wa ofisi na katiba ya chama cha wawendesha bodaboda pikipiki manispaa ya
Morogoro CHAWAPIMAMO ambapo alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya waendesha
bodaboda hao kusababisha vifo kwa abiria wao kwa kupata ajari na hata wakati
mwingine kuwaua kwa kudhania kuwa wana mali.
Abood alisema ni vyema
waendesha bodaboda hao wakawa na tabia ya kuaminika kwa watu
wanaowabeba,uadilifu na kujiweka katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja kuwaeshimu askari wa usarama
barabarani.
Pia mbunge huyo
aliwataka viongozi wa CHAWAPIMAMO kuongoza kwa kufuata katiba na wawe wenye
kutoa taarifa za mapato na matumizi mara kwa mata katika vikao vyao ili
kuwepuka minung’uniko isiyokuwa ya lazima kutoka kwa wanachama.
“Kuanzishwa kwa chama
hiki kusiwe chanzo cha migogoro hasa ninyio viongozi msiwe wenye kuabudiwa na mnajiona
kama miungu watu kwa wenzetu kwani hiki ni chama cha wananchama fanyeni kazi
kwa kufuata misingi mliojiwekea,”alisema
Akisoma risala katika
uzinduzi wa chama hicho katibu wa CHAWAPIMAMO Juma Bega alisema kuwa chama
kilianzishwa 2009 kikiwa hakina ofisi na kwamba mpaka sasa kina wanachama zaidi
ya 400 ambao ni waendesha bodaboda,kimekuwa kikishirikiana na jeshi la polisi
kitengo cha usalama barabarani kutoa mafunzo juu ya usalama na udereva kwa
waendesha bodaboda hao.
Bega alisema kuwa
kuanzishwa kwa chama hicho kumesaidia kukuza ajira na kipato kwa vijana,biashara
kuongezeka pamoja na kupunguza ajari za mara kwa mara za barabarani.
Alisema mamlaka ya
mapato Tanzania TRA pamoja na kuondoka kodi mapato katika pikipiki kumekuwa na changamoto
inayokabiliana ambayo ni kutozwa ghalama kubwa ya kodi ya leseni ya barabara (Motor
vehicle Licence) na kilalamikia kutakiwa kuweka mtungi wa gesi ambao hawaoni
sehemu ya kuuweka.
Aidha alisema matarajio
yao ni kuanzisha mfuko wa kusaidiana nia ikiwa ni kusaida pale mwenzao anapopata
ajari ama kufariki kutokana na chombo anachokiendesha pikipiki ama vinginevyo.
Katika uzinduzi wa
ofisi na katiba cha chama hicho mbunge Abood alitoa msaada wa pikipiki 5 aina
ya TOYO yenye thamani ya shilingi 8 milioni ambazo alizitoa kambo chanzo cha
mapato cha chama hicho ambapo aliwataka kukopeshana na kuzalisha.






0 comments:
Post a Comment