MELI AMBAYO INA KLINIKI YA UTOAJI MIMBA YA UHOLANZI.
MELI moja ya Uholanzi iliyokuwa
ikielekea katika pwani ya Morocco kutoa huduma ya utoaji mimba kwa
wanawake imezuiliwa kuingia bandarani kwa mujibu wa wanaharakati
walioituma nchini humo.
Kundi la wanaharakati hao wanawake linasema kuwa
bandari ya Smir imefungwa kabisa na meli za kivita zinalinda doria eneo
la bandari hiyo.
Hapo jana Morocco ilisema kuwa meli hiyo
haijapewa mualiko na mamlaka zinazotambuliwa nchini humo na hivyo
ilikuwa ikifanya shughuli hiyo kinyume cha sheria.
Sheria za Morocco zinakataza utoaji mimba isipokuwa tu iwapo maisha ya mwanamke mjamzito yako hatarini.
Ibtissame Lachgar, ambaye ni mmoja wa
wanaharakati wanaotetea haki ya utoaji mimba amesema wanawake wengi
wanalazimika kufanya utoaji mimba kwa njia zisizo rasmi ambazo ni
hatari.
0 comments:
Post a Comment