JKT RUVU.
KLABU ya soka ya Polisi Moro SC imeendeleza kusuasu katika ligi kuu Tanzania bara baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prinson katika mchezo mkali na kusisimua liofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Dalili za kupoteza mchezo huo zilianza mapema baada ya Prinson kutawala mchezo dakika chache tangu kuanza na Polisi kuzinduka dakika ya tatu na kujipatia bao la kuongoza lilifungwa na PaungoNywange kwa mkwaju wa penalti.
Prinso hawakukataa na kuendeleza mashambulizi na katika dakika ya 52 Peter Michael aliisawazishia timu yake bao kwa njia ya mkwaju wa penalti na kuongeza bao la pili katika dakika ya 77 baada ya walinzi wa Polisi Moro kufanya uzembe wa kuondoa mpira katika eneo la hatari na kufungwa bao hilo lililofungwa na Jhn Matei.
Katika mchezo mungine Maafande wa Kujenga Ta4fa leo JKT Ruvu leo wamefanikiwa kutoka na
ushindi baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo na kuzuia kujiuzulu
kwa Kocha wake.
Kocha wa JKT Ruvu baada ya kufungwa na Azam FC goli 3 na kufikisha michezo mitatu wakipoteza alisema endapo angepoteza mchezo wa leo dhidi ya Mgambo Shooting uliochezwa leo katika uwanja wa Azam angejiuzulu.
JKT Ruvu wameifunga goli 1-0 Mgambo Shooting goli lililofungwa katika dakika 71 kupitia kwa Haruna Adolf na kuzidi kuwa weka mahali pabaya Mgambo Shooting iliyopoteza michezo yote mitano ya ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment