BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TATIZO LA MWANANCHI KUISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU BADO HALIJAPATIWA UFUMBUZI


KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijah, amesema pamoja na jitihada za serikali kuwakwamua wananchi kutoka katika hali ngumu ya maisha, bado tatitizo linalowakabili la kuishi chini ya dola moja halijapatiwa ufumbuzi wa kutosha.

Kijah alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, mbele ya mgeni rasmi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, wakati wa uzinduzi wa mpango wa majadiliano wa maendeleo wa Millenium 2015.
 
Alisema tatizo hilo ambalo lina wakabili Watanzania waliowengi linahitaji majadiliano mapana yenye lengo la kuleta mafanikio ya haraka kwa wote, ndani ya kipindi hicho kilichobaki cha kuelekea mwaka 2015.
 
“Katika mambo saba ya milenium ni ukweli katika hili la kuwakwamua wananchi kutoka katika maisha ya dola moja hatuja fanikiwa bado juhudi zetu ni muhimu katika kulimaliza”alisema Kijah.
 
Akifafanunua alisema katika malengo saba ya mileniam, Tanzania imefanya vizuri upande wa elimu kwani imeweza kuandikisha wanafunzi wengi katika elimu ya msingi na sekondari.
 
Hata hivyo, bado kunachangamoto zinazoikabili elimu ambapo ubora wake haujakuwa wakurudhisha hivyo juhudi zinahitajika katika kuimarisha ili iyendane na ubora unaotakiwa.
 
Kijjah alisema hali hiyo inatokana na uhaba wa walimu wa kutosha, vifaa vya kufundishia pamoja na nyumba za walimu ambazo ni tatizo linalowafanya walimu wengi kukimbia maeneo waliyopangiwa kufanyakazi.
 
Kwa upande wa afya, alisema ingawa vifo kwa watoto chini ya miaka mitano na mama wajawazito vinaendelea kupungua lakini bado yapo matatizo yanayohitaji ufumbuzi.
 
Naye mgeni rasmi, Balozi Sefue alisema Tanzania ni moja kati ya nchi 50 duniani iliyochaguliawa na umoja wa mataifa ili kujadili mpango huo, changamoto za mileniam 2015, ambapo mpango huo utawashirikisha wadau wote kutoka ngazi ya kijiji hadi taifa kwa lengo la kutoa maoni yatakayosaidia katika kujiletea maendeleo yao.
 
Alisema suala la maendeleo ya wananchi siyo la serikali pekee bali ni wajibu wa kila mdau wa nchi hii, hivyo wajitokeze katika katika kushiriki, kutoa mchango wa mawazo kwa ajili ya mpango huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: