Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas)
MZEE mwenye umri wa miaka70,aliyetambulika kwa jina Jumbe Lolida mkazi wa King’ori ,Arumeru Mkoani Arusha ,amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara alipokuwa akitembea miguu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas kwa waandishi wa habari,tukio hilo limetokea jana majira ya saa1.30 na kulihusisha gari aina ya Suzuki lenye namba T 844 AQT .
Alisema gari hilo lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Benson Onesmo Lyimo (41) mkazi wa Mgadirisho wilaya ya Arumeru na lilikuwa likitokea mjini Moshi kuelekea Usa River na kwamba lilipofika eneo la king’ori ndipo alipokutana na marehemu huyo akijaribu kuvuka barabara na kumgonga.
Kamanda Sabas alifafanua kuwa mara baada ya tukio hilo dereva wa gari hilo alifanikiwa kutoroka na kutokomea kusikojulikana na polisi wameanzaisha msako na pindi atakapopatikana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi zaidi .
0 comments:
Post a Comment