BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VURUGU ZA WAISLAM MBAGALA.

 



ENEO la Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam jana liligeuka uwanja wa mapambano kati ya makundi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Waislamu na polisi baada ya watu hao kuvamia Kituo cha Polisi Kidogo cha Maturubai kilichopo eneo hilo.

Watu hao walivamia kituo hicho wakitaka wakabidhiwe mtoto anayedaiwa kukojolea kitabu kitakatifu cha Quran ili wamwadhibu.
Vurugu hizo zilizoanza tangu saa nne asubuhi, zilisababisha makanisa matano kuchomwa moto, magari kadhaa kuvunjwa vioo na watu hao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema watu kadhaa wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo... “Siwezi kutaja idadi ya waliokamatwa, lakini kuna watu tunawashikilia kutokana na kufanya fujo, kwa sasa niko katika operesheni, nitazungumza kwa kirefu baadaye.”

Hata hivyo, Misime alisema hakuna kifo kilichotokea wala majeruhi.

“Pamoja na kwamba bado tupo katika eneo la tukio bado hatujashuhudia vifo wala majeruhi na tunaomba Mungu mambo hayo yasitokee.

Aliyataja makanisa hayo kuwa ni la TAG Kizuiani, Wasabato Kizuiani, TAG la Shimo la Mchanga na KKKT Mbagala Zakheim.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchomaji wa makanisa hayo ni kosa la jinai na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao.

Alisema katika vurugu hizo gari la Mkuu wa Polisi Wilaya ya Temeke (OCD) limevunjwa vioo.

Kamanda Kova alisema Jeshi hilo litaimarisha ulinzi katika makanisa hayo ili kuhakikisha kunakuwa na usalama.

Miongoni mwa magari hayo matano yaliyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo zilisababisha Barabara ya Kilwa kufungwa kwa muda ni gari la Kituo cha Televisheni cha Clouds ambalo lilivunjwa vyoo.

Akizungumzia suala hilo, mkazi wa Mbagala Mission, Nassor Mohamed alisema vurugu hizo zilitokea baada ya mtoto mmoja kukojolea Quran.

Alisema mtoto huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuwapo na ubishi na mtoto mwenzake ambaye wanasoma wote katika Shule ya Sekondari Chamazi.

Mohamed alisema mtoto huyo mwenye miaka 14, alikuwa akibishana na mwenzake mwenye umri kama huo kwamba mtu akikojolea kitabu hicho hugeuka kuwa nyoka.

Alisema kuwa mtoto huyo aliamua kufanya kitendo hicho ili kuona kama atageuka nyoka na wakati akifanya kitendo hicho mzee mmoja alimuona na kumhoji kisha kumpeleka kwa mama yake na kumshtaki.

“Yule mama aliwajibu kuwa kama ni hilo tu, basi awape hela wakanunue kingine. Aliposema hivyo wale watu wakakasirika wakamwambia, sisi tulikuja kukuambia kwa uzuri ili umwadhibu mwanao, lakini kutokana na majibu yako hatukuachii tena huyu mtoto,” alisema.

Alisema baada hapo, watu hao walimpeleka mtoto huyo katika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Chamazi ambako waliandikiwa barua na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kilichopo katika eneo hilo.

Jumatano jioni, watu hao walifika katika kituo hicho wakitaka wapewe tena mtoto huyo na ndipo walipoambiwa kuwa amehamishiwa katika Kituo cha Maturubai.

Alisema baada ya kumkosa mtoto huyo walihamasishana na kukubaliana kuwa baada ya kutoka msikitini kesho yake (jana), wakavamie kituo hicho na kumtoa mtoto huyo.

Wakati ghasia hizo zikiendelea, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Temeke, Farid Salehe aliwasihi waumini wa dini hiyo kuwa watulivu.

Katibu wa Vijana wa Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkarim Kulao aliwataka Waislamu waliokuwa wamekusanyika katika eneo la kituo hicho cha polisi kurejea majumbani kwao kwani mtuhumiwa huyo alikuwa ameshahamishwa.

Baadaye Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha baadhi ya watu waliokuwa wamekiendelea kubaki katika eneo hilo.

Askari waliokuwa na mabomu ya machozi walitawala eneo hilo kuweka ulinzi na hatimaye kufanikiwa kuwatawanya watu hao.
Baada ya kutimuliwa katika mkusanyiko huo, kundi moja la watu hao lilifika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mbagala na kulichoma moto.

Mzee wa Kanisa hilo, Siaga Kiboko alisema mali kadhaa zimeharibika na kwamba walishatoa taarifa polisi.
Nyongeza na Raymond Kaminyonge.

VURUGU ZA WAISLAM MBAGALA KATIKA PICHA.

  Baadhi ya waandamanaji wakiwa jirani na Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala jijini Dar leo.
    Baadhi ya maafisa wa polisi wakinawa maji baada ya mabomu ya machozi kupigwa.
   Gari la  Kampuni ya…
  Baadhi ya waandamanaji wakiwa jirani na Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala jijini Dar leo.
    Baadhi ya maafisa wa polisi wakinawa maji baada ya mabomu ya machozi kupigwa.
   Gari la  Kampuni ya Clouds Media Group likiwa limepasuliwa kioo cha nyuma.
  Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Ally Ramadhani ambaye ni dereva wa daladala naye akiwa ameambulia kipigo baada ya kujichanganya na waandamanaji.
    …Dereva Ally Ramadhani akisikilizia maumivu.
     Mmoja wa waandamanaji.
     Baadhi ya waandamanaji wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi.
Kanisa la Sabato Mbagala Kizuiani likiwa limevunjwa vioo.
…Vioo vilivyovunjwa kanisani hapo.
…kanisa hilo la Sabato.
  ...Muonekano wa kanisa hilo la Sabato.
    Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Paul Martin ambaye alidai alikuwa akienda sokoni ndipo akaambulia kipigo.
Kanisa la Aglikana ambalo pia lilishambuliwa na waandamanaji.
…Anglikana.
   Mabenchi ya kanisa la Anglikana yakiwa yametupwa nje.
Kibao cha kanisa kikiwa kimevunjwa.
  Muonekano wa kanisa hilo la Anglikana.
Gari lililokuwa ndani ya Kanisa la T.AG Mbagala Kizuiani likiwa limevunjwa vioo.
 
…Hili lilichomwa moto.
Baadhi wa waumini wa kanisa la T.A.G wakililinda kanisa lao.

WATU wanaodaiwa kuwa ni Waislamu wamevamia makanisa mbalimbali yaliyopo Mbagala Kizuiani jijini, Dar 
wakihamasisha vurugu wakimtuhumu mtoto Emmanuel Josephat kuwa amekojolea kitabu cha dini hiyo (Msaafu) Oktoba 10, mwaka huu.
 
Baadhi ya makanisa yaliyoshambuliwa ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto magari yao ni  Kanisa la Sabato, Aglikana na T.AG .
 
(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: