WAZIRI mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alisema Uturuki inataka amani na usalama katika kanda hiyo na haina nia ya kufanya vita.
Erdogan aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na makamu wa rais wa Iran, Mohammed Reza Rahimi ambaye yuko ziarani nchini Uturuki.
Maoni hayo ya Erdogan yanakuja siku moja baada ya Syria kurusha makombora katika mji wa Akcakale, nchini Uturuki, na kusababisha vifo vya raia watano wa Uturuki na wengine 10 kujeruhiwa.
Baada ya Shambulizi hilo la Syria bunge la Uturuki lilifanya mkutano wa dharura na kupitisha uamuzi wa kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria siku ya Alhamisi katika maeneo ya mpakani, kwa kura 320 za ndio na kura 129 za hapana.
0 comments:
Post a Comment