
RAIS Omar Hassan al Bashir amesema Israel ni adui Nambari moja wa Sudan na kukariri madai ya Khartoum kwamba utawala wa Kizayuni ulitekeleza mashambulizi ya anga mwezi Oktoba dhidi ya kiwanda cha kutengeneza silaha katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Al Bashir amebainisha kuwa, Israel ni adui nambari moja wa Sudan na kwamba wataendelea kuuchukulia utawala huo kama adui yao.
Rais wa Sudan aidha amesema, hatua hiyo ya Israel inaonyesha kuongezeka wasiwasi wa utawala huo kuhusiana na mwamko wa kisiasa na kijamii katika eneo na kuendelea taifa la Sudan.
Oktoba 24 Waziri wa Habari wa Sudan Ahmed Bilal Osman alisema kuwa, ndege 4 za jeshi la Israel zilishambulia kiwanda cha silaha mjini Khartoum na kuua watu wasiopungua wawili. Sudan pia ililitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani mashambulizi hayo ijapokuwa hadi sasa baraza hilo halijafanya hivyo.

0 comments:
Post a Comment