
Mtawa aliyejiteketeza kwa moto kuonyesha kero na China.
WANAHARAKATI nchini China wanasema kuwa vijana watatu watawa wa Tibet pamoja na mama
mmoja walijiteketeza mkesha wa kongamano la chama cha tawala cha
kikomunisti nchini China.
Shrika la Free Tibet linasema kuwa mmoja wa
watawa hao alifariki katika kile inachosema ni idadi kubwa ya watu
kujiteketeza kama njia ya kuonyesha kukerwa na utawala wa china.
Matukio ya hivi karibuni ya watu
kujiteketeza moto katika maeneo ya china yaliyo na watu wa Tibet
yamefikisha idadi ya watu hao wanaojiteketeza kuwa zaidi ya watu sitini
tangu mwaka jana.
Wengi wao wamefariki. Na huenda kuna umuhimu katika wakati ambapo visa hivi vimetokea.
Kuimarishwa kwa usalama kote China kwa kongamano
la chama tawala cha kikomyunisti nchini, hakujazuia malalamiko ya raia
wa Tibet dhidi ya utawala wa China. Badala yake yameongezeka.
Wanaharakati wanasema idadi ya watu kujiteketeza kwa muda wa siku moja, hii leo, haikutarajiwa.
Tangu mwaka jana zaidi ya raia sitini wa Tibet
wameamua kutumia njia kubwa kabisa ya kuonyesha kuvunjwa moyo, kwa kile
wanachosema ni ukandamizaji wa China kwa tamaduni zao.

Raia wa Tibet wanaopinga China.
Maafisa wa serikali wa China wametoa fedha
katika maeneo yaliyo na raia wa Tibet na wameendelea kukana tuhuma hizo
za ukandamizaji.
Mkurugenzi wa kundi linalotetea kuachiwa huru
maeneo ya Tibet, amesema malalamiko ya hivi karibuni yananuiwa kutoa
ishara kwa kizazi kipya cha uongozi China, kitakachoidhinishwa katika
kongamano linaloendelea Beijing, kuwa raia wa Tibet wataendelea
kupigania uhuru wao.
Baadhi ya raia wa Tibet walio uhamishoni,
wanatumai kuwa mwanamume anayedokezwa kuwa kiongozi mpya, Xi Jinping,
huenda akawapatia nafasi ya kufanyika mabadiliko.

0 comments:
Post a Comment