Baadhi ya askari jeshi wa kundi la M23
Mapigano ambayo yalizuka baina ya Jeshi la FARDC na Wapiganaji
wa Kundi la M23 yanatajwa kusababisha vifo vya watu mia moja na hamsini
wakiwemo wapiganaji wa waasi na Afisa mmoja wa Jeshi.
Msemaji wa Jeshi la FARDC Olivier Hamuli amesema wamefanikiwa
kuwafurusha wapiganaji wa Kundi la M23 na sasa hali ya utulivu
imeimarishwa na amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao.
Mapigano hayo yamezuka kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo DRC Augustin Matata Ponyo akiwa ziarani nchini
Ufaransa na amekiri wanahitaji msaada wa nchi hiyo kurejesha amani huko
Kinshasa.
Katika hatua nyingine Msemaji wa Kisiasa wa M23 Betrand Bisimwa
amejitokeza na kukanusha madai ya wao kuwatishia maisha waandishi wa
habari huko Goma.
Rwanda kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Louise Mushikiwabo ametoa
wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo baina ya FARDC na M23 na kuwataka
waheshimu maafikiano yaliyotolewa na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu ICGLR.

0 comments:
Post a Comment