BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAREKANI NA AU WAKATA WAAASI WA KUNDI LA M23 WADHIBITIWE GOMA DRC.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton(R) na mwenyekiti wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma(L)
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton(R) na mwenyekiti wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma(L).
 
MAREKANI na Umoja wa Afrika zinahimiza hatua ichukuliwe mara moja  ya kupelekea kikosi kisichoegemea upande wowote katika maeneo ya mashariki mwa Congo yanayokaliwa na waasi kwenye mpaka  wa nchi hiyo na Rwanda.

Waziri wa  mambo ya nje  wa Marekani, Hillary Clinton amesema ni sharti Rwanda  isaidie  kuzuia uungaji mkono wa uasi huo.  
 
Kundi la waasi hao wa M23 limesema linajiandaa kuondoa udhibiti wake kwenye mji wa Goma, lakini maafisa wa Marekani wamesema ni mapema mno kubaini ikiwa kundi hilo linaondoka au lina mpango mwingine wa kijeshi.

Katika mkutano uliofanyika kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani akiwa na mwenyekiti wa  Umoja wa  Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, Waziri Clinton amesema njia pekee kwa waasi hao ni kutii mkataba uliofikiwa nchini Uganda.  
 
Kama sehemu ya mkataba huo, Rais wa Congo Joseph Kabila, Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda walikubaliana juu ya kupelekwa kikosi kisichoegemea upande wowote kuchukua udhibiti wa maeneo yanayokaliwa na waasi.

Lakini mkataba huo umegubikwa na utata kwa sababu kuna dhana kuwa Rwanda ndiye muungaji mkono mkuu wa waasi hao wa M23, dai ambalo Rwanda inakanusha.  
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dlamini Zuma anasema  kuungana pamoja kwa viongozi wa ukanda huo kuzima mapigano ni muhimu zaidi kuliko kulaumiana. 
 
Waziri Clinton pia alisisitiza kuwa sharti viongozi wote wachukue  hatua kuzuia kundi hilo la waasi kupata uungaji mkono wa aina yoyote ile.

Mapigano mashariki mwa Congo yamepelekea watu 285,000 kukimbia nyumba zao katika muda wa miezi minane iliyopita  na kusababisha kile waziri Clinton anasema ni madhara makubwa ya kibinadamu huku wafanyakazi wa afya  huko Goma wakiuawa na hata wengine kutekwa nyara.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: