TAASISI ya Utafiti ya Synovet imeweka hadharani matokeo ya utafiti wao kuhusu vyombo vya habari nchini kwa mwaka 2012, unaoonyesha kwamba magazeti yote matatu ya Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, MCL, yanaongoza kwa kuwa na wasomaji wengi.
MCL ndiyo wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.
Kwa mujibu wa utafiti huo, kwa magazeti ya Kiswahili ya kila siku, Mwananchi limeyaacha mbali magazeti mengine ikiwa ni zaidi ya nusu ya wasomaji wanaofikia asilimia 59.
Kwa upande wa magazeti ya Kiingereza, utafiti unaonyesha Watanzania wanaosoma magazeti ya Kiingereza ni karibu asilimia 10 tu, na kati ya hao, asilimia nne wanasoma Gazeti la The Citizen, huku magazeti mengine yote ya kiingereza yakigawana 6% zilizobaki.
Gazeti la Mwanaspoti linayaongoza magazeti zaidi ya 10 ya michezo yanayochapishwa hapa nchini kwa kusomwa na asilimia 31 ya wasomaji wa habari za michezo nchini na gazeti lingine linafuatia kwa kusomwa kwa asilimia 20 tu.
Magazeti ya michezo yaliyobaki yanagawana asilimia 49.
Kwa mujibu wa Synovet, kinachowavutia zaidi wasomaji kuyasoma magazeti ya MCL ni pamoja na ubora wa habari, muundo wa gazeti, na uhakika wa ukweli wa habari zinazoandikwa na magazeti haya.
Utafiti huu pia umewagusa
wafanyabiashara, kampuni na taasisi mbalimbali ambazo wengi wao
wamejikuta wakimiminika kutaka kutangaza biashara zao na magazeti haya
baada ya kugundua ukweli wa kisayansi kwamba matangazo yao yatawafikia
wasomaji wengi zaidi wanapotangaza katika magazeti ya MCL na kupata
matokeo wanayoyatarajia.
0 comments:
Post a Comment