Mtuhumiwa namba moja wa biashara haramu ya kusafirisha na kuuza nyara za
serikali,Pembe za ndovu,Hong Kong China,Hasan Othman (Hasnoo) kipelekwa
kizimbani kusomewa mashitaka yanayomkabili yeye na wengine kwenye
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Dar es salaam jana. MWENYEKITI wa Chama cha Soka Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama Hasanoo (43) na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la uhujumu uchumi na kusafirisha pembe za ndovu (Meno ya Tembo) kutoka Dar es Salaam kwenda Hong Kong, yenye thamani ya Sh1.1 bilioni.
Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro jana aliwataja
washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi,
Augustina Mmbando kuwa ni Ally Kimwaga, Dastan Mwanga, Godfrey Mwanga,
John Mlai na Khalid Fazaldin.
Kimaro alidai katika shtaka la kwanza kuwa, kati
ya Septemba Mosi na Novemba 20, mwaka huu, Dar es Salaam na Hong Kong
kinyume na kifungu cha 384 ya kanuni ya adhabu sura ya 16.
Amesema washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama
ya kujihusisha na biashara ya nyara za serikali bila ya kuwa na leseni
inayowaruhusu kufanya hivyo.
Katika shtaka la pili, Kimaro alidai kuwa kati ya
Septemba Mosi na Novemba 20, mwaka huu, Dar es Salaam na Hong Kong
washtakiwa hao kwa nia ovu walipanga, wakatekeleza, wakasimamia na
kuwezesha kifedha kufanyika kwa biashara ya nyara za serikali kwa
kusafirisha vipande 569 vya Pembe za ndovu, vyenye uzito wa kilogramu
1330 na thamani ya Sh 1,185,030,000 kwenda Hong Kong.
Wakili huyo wa Serikali, katika shtaka la tatu
alidai kuwasiku hiyo ya tukio washtakiwa hao walijihusisha na biashara
ya nyara za serikali kinyume na kifungu cha 80 na 34 ya uhifadhi wa
Wanyama Pori namba 5.
Aliongeza kwa kudai kuwa, washtakiwa hao kwa nia ovu waliendesha biashara hiyo ya nyara za serikali bila ya kuwa na kibali halali kinachowaruhusu kufanya biashara hiyo.
Aliongeza kwa kudai kuwa, washtakiwa hao kwa nia ovu waliendesha biashara hiyo ya nyara za serikali bila ya kuwa na kibali halali kinachowaruhusu kufanya biashara hiyo.
Baada ya kuwasomea washtakiwa hao mashtaka, Hakimu
Mmband aliwaambia washtakiwa hao kuwa, kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu
Mkazi, Ritha Tarimo ambaye hayupo na kwa sababu hiyo, hawaruhusiwi
kuongea chochote kwa sababu hati ya mashtaka haijaambatanishwa na hati
kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Wakili Kimaro alidai kuwa upelelezi wa kesi bado haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Mmbando aliiahirisha kesi hiyo, hadiJumatano ya Novemba 28, mwaka huu itakapotajwa.
Mbali na kesi hiyo, Hasanoo aliyewahi kuwa
kiongozi wa Simba pia anakabiliwa na kesi nyingine ya wizi wa tani
26.475 za madini aina ya Shaba zenye thamani ya Sh333, 467,848.13 kutoka
Zambia kinyume na kifungu cha 258, 265 na 269 (c) vya kanuni ya adhabu
mali ya Kampuni ya Liberty Express Tanzania Ltd.

0 comments:
Post a Comment