RIPOTI mpya iliyotolewa na shirika la Save the
Children linaonya kuwa pengo kati ya watu maskini na matajiri imekuwa
kubwa sana katika miaka yake 20 tangu kuanza.
Shirika hilo linasema kuwa pengo hilo limekuwa kubwa na linawaathiri zaidi watoto.
Kwa mujibu wa Save the Children, linasema kuwa
hali ya vifo vya watoto wachanga imepungua ingawa katika sehemu zingine
bado kuna changamoto.
Ripoti yenyewe ambayo inakuja kabla ya mkutano
mkuu wa umoaj wa mamataifa kuhusu umaskini, inasema kuwa huenda hatua za
hali ya kuimarika zikaathirika ikiwa hali hiyo haitashughulikiwa vyema.

0 comments:
Post a Comment