Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
amemsimamisha kazi kwa muda Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavula nchi hiyo,
baada ya Umoja wa Mataifa kumtuhumu Jenerali Gabriel Amisi Kumba
kuwasaidia waasi na makundi yanayobeba silaha dhidi ya serikali ya
Kinshasa.
Hata hivyo serikali ya Kongo imeanzisha uchunguzi wa kina
kubaini tuhuma hizo zilizotolewa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Jenerali
Gabriel Amisi Kumba za kuwasaidia waasi wa nchi hiyo.
Kwa upande mwengine, wakati waasi wa mashariki mwa Kongo wakizidi
kusonga mbele katika eneo hilo, Jean Marie Runiga Lugerero kiongozi wa
waasi wa March23 ameelekea Kampala mji mkuu wa Uganda kwa shabaha ya
kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa nchi hiyo juu ya
mgogoro wa mashariki mwa Kongo.
Waasi wa M23 jumanne iliyopita
waliudhibiti kikamilifu mji wa Goma, makao ya Jimbo la Kivu na Kaskazini
na hivi sasa wanasonga mbele kuelekea upande wa kusini mwa mji huo.

0 comments:
Post a Comment