Mshambuliaji wa Klabu ya Simba Emmanuel Okwi katikati akitafuta mbinu ya kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar, Jamali Simba kulia na Hussein Ramadhani kushoto wakati wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar ilishinda bao 2-0.
KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KILICHOTOA KICHAPO KWA KUITANDIKA SIMBA BAO 2-0 KATIKA LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.
KIKOSI CHA SIMBA KILICHOTANDIKWA BAO 2-0 NA MTIBWA SUGAR LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.
Benchi la ufundi la klabu ya Mtibwa Sugar likiongozwa na kocha mkuu wa klabu hiyo Meck Mexime kulia muda mfupi kabla ya vijana yake kuiadhibu Simba kwa kuwapa kipigo cha bao 2-0 katika ligi kuu ya vodacom Tanzania bara kutoka kwa Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Benchi la ufundi la klabu ya Simba likiongozwa na kocha mkuu Milovan Cirkovic kushoto muda mfupi kabla ya timu yake kupokea kipigo cha bao 2-0 katika ligi kuu ya vodacom Tanzania bara kutoka kwa Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Sehemu ya jukwaa la wazi la mashabiki mchanganyiko nao wakifuatilia mchezo huo ambao umeishia kwa Simba kukubali kufungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar.
Jukwaa la klabua ya Simba wakiwa wanafuatilia mchezo baina ya timu yao na Mtibwa Sugar baada ya kupokea kipigo cha bao 2-0.
Nahodha wa Klabu ya Simba Juma Kaseja akiwaongoza wachezaji wenzake kuwasalimia wachezaji wa Mtibwa Sugar.
Mwamuzi wa kati Judith Gamba kutoka Arusha (mwenye mpira) akiwaongozawachezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar Manungu Turiana na Simba katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara uwanja wa Jamhuri Morogoro.











0 comments:
Post a Comment