BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TRA YAJIVUNIA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya. 
WAFANYABIASHARA mkoani Iringa wamepongezwa kwa ulipaji kodi na kufuata taratibu na sheria za ukusanyaji wa mapato.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa, Rosalia Mwenda alisema ulipaji mzuri wa kodi umesababisha kuongezeka kwa makusanyo ya mapato na kuvuka lengo lililowekwa.

Mwenda alisema wafanyabiashara hao wamekuwa mstari wa mbele katika ulipaji wa mapato kwa wakati na kusababishia serikali kufanikisha malengo iliyojiwekea.
Alisema mwaka uliopita mkoa ulipangiwa kukusanya Sh23 bilioni, lakini walivuka lengo na kukusanya Sh24 bilioni sawa na asilimia 105.

Alisema hayo ni mafanikio makubwa na kwamba, mwaka huu wa fedha wamepangiwa Sh33 bilioni na watafanikiwa kwa sababu wamejipanga.

Meneja huyo alisema ili kuhakikisha wafanyabishara wanafanikiwa katika biashara zao, hasa kufahamu taratibu za sheria na jinsi ya kutumia vifaa vyao katika kudhibiti mapato, tayari  wametoa semina kuwaelmisha sheria hizo.

Mwenda alisema mfanyabiashara anayeingiza Sh4o milioni ndiye anayetakiwa kutumia mashine ya elektoniki.

Pia, alisema katika mwaka huu wa fedha bado mkoa unadai madeni ya zaidi ya Sh1 bilioni, ambayo wameyawekea mkakati wa kuyafuatilia ili yalipwe.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: