
Jengo la Bunge la Marekani, Washington DC
UCHAGUZI mkuu Marekani umemalizika huku kukiwa na mabadiliko kiasi ya viti vya bunge, uwiano wa madaraka kati ya baraza la Seneti na bunge unabaki kuwa vile vile.
Katika baraza la seneti chama cha Democrat kimeongeza angalau kiti kimoja na chama cha Republican kimepoteza kiti kimoja, hii ikimaanisha kuwa baraza la seneti mwaka 2013 litakuwa na wademocrat wasiopungua 51, wa-Republicans wasiopungua 44 na angalau viti viwili vya wabunge wa kujitegemea.
Viti vitatu bado havijajulikana vitakuwa vinaegemea chama gani.
Akizungumza na Sauti ya Amerika, Professa Julius Nyang’oro wa chuko kikuu cha North Carolina alisema Wademocrat wamepiga hatua kubwa katika baraza la seneti ambapo jimbo la Massachusetts, m-Democrat Elizabeth Warren alimshinda Seneta wa sasa Scott Brown kutoka chama cha Republican.
Chama cha Democrat kimechukua ushindi pia katika jimbo la Virginia lenye upinzani mkali, ambapo gavana wa zamani wa Democrat Tim Kaine alimshinda gavana wa zamani wa Republican, George Allen.

0 comments:
Post a Comment